Waziri Lukuvi Amemaliza Mgogoro Wa Ardhi Uliodumu Zaidi Ya Miaka Saba Pwani
HomeHabari

Waziri Lukuvi Amemaliza Mgogoro Wa Ardhi Uliodumu Zaidi Ya Miaka Saba Pwani

 Na. Hassan Mabuye, Pwani Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amemaliza mgogoro wa Ardhi kati ya mwekezaj...


 Na. Hassan Mabuye, Pwani
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amemaliza mgogoro wa Ardhi kati ya mwekezaji wa Kampuni ya Dimara na  wakazi wa Kijiji cha Kisabi wilaya ya Kibaha mkoani Pwani uliodumu kwa zaidi ya miaka Saba.

 Waziri Lukuvi amemaliza mgogoro huo wakati akiwa katika ziara ya kutembelea maeneo yenye migogoro ya ardhi katika mkoa wa Pwani.

Akiwa katika Kijiji hicho Lukuvi alitoa maelekezo ya wavamizi wote waliojimilikisha sehemu ya eneo hilo kuondolewa na kupewa eneo katika shamba la ekari 51 lililorudishwa Serikalini hivi karibuni.

Lukuvi alitoa maelekezo kwa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha kufufua mipaka ya eneo hilo na kuweka katika matumizi mazuri ya ardhi kupima viwanja na kuviuza kwa kushirikiana na mmiliki.

“sipo tayari kuwavumilia wavamizi kwenye maeneo yanayomilikiwa kihalali na nimeamua kuja Pwani kwakua mnaongoza kwa kuvamia maeneo bila kufuata sheria, kazi yangu ni kuwalinda wanaomiliju ardhi kisheria na kimila nataka nirudishe heshima” alisema Mhe. Lukuvi.

Alisema wananchi hao watapewa maeneo kwenye ekari 51 za shamba ambalo lilifutwa umiliki wake na Mhe. Rais na kurudishwa Serikalini na wanalazimika kulipa gharama za hati miliki baada ya viwanja kupimwa katika Halmashauri ya Kibaha.

Waziri Lukuvi pia alitoa maelekezo kwa wakuu wa mikoa na wilaya kutembelea maeneo yenye migogoro ya ardhi na kuondoa wavamizi ili kukomesha tabia hiyo.

Alitoa onyo kwa maofisa ardhi kuhakikisha wanapopeleka majina ya maeneo ambayo hayajaendelezwa kwa Waziri watende haki kwa kuwa na ushahidi kutoka kwa mkuu wa wilaya atakayekiuka hatua zitachukuliwa.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani alizindua kampeni ya kutokomeza migogoro ya ardhi mapema wiki hii lengo kumaliza migogoro iliyopo na kukomesha uvamizi kwenye maeneo yanayomilikiwa kisheria katika mkoa huo.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Waziri Lukuvi Amemaliza Mgogoro Wa Ardhi Uliodumu Zaidi Ya Miaka Saba Pwani
Waziri Lukuvi Amemaliza Mgogoro Wa Ardhi Uliodumu Zaidi Ya Miaka Saba Pwani
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi7TmyGl91UnlBfehnz7ZGAtIvdGcHS6llInxczHzD-uM9vv1g5dlETbkIwYpiMjInTLhhfkCYJ55e95pTh9HIQWzJFdSVRnMMlhcwys_TwLQVfHN3iLeD1AUpZgdjeBPoMaeXcjyVNhZv7/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi7TmyGl91UnlBfehnz7ZGAtIvdGcHS6llInxczHzD-uM9vv1g5dlETbkIwYpiMjInTLhhfkCYJ55e95pTh9HIQWzJFdSVRnMMlhcwys_TwLQVfHN3iLeD1AUpZgdjeBPoMaeXcjyVNhZv7/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/waziri-lukuvi-amemaliza-mgogoro-wa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/waziri-lukuvi-amemaliza-mgogoro-wa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy