Wananchi Wasisitizwa Kufanya Uhakiki Wa Laini Za Simu
HomeHabari

Wananchi Wasisitizwa Kufanya Uhakiki Wa Laini Za Simu

Na Mwandishi wetu, Dodoma Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile ametoa rai kwa wananchi kuendelea k...


Na Mwandishi wetu, Dodoma
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile ametoa rai kwa wananchi kuendelea kufanya uhakiki wa laini za simu kwa lengo la kutambua laini zilizosajiliwa kwa majina yao ili kuepuka kuhusishwa na makosa ya utapeli mitandaoni.

Hayo ameyazungumza katika hafla fupi ya uzinduzi wa tovuti na Mpango mkakati wa Wizara hiyo wa miaka mitano kuanzia mwaka 2021/22 hadi 2025/26 uliofanyika jijini Dodoma

Amesema kuwa  ni muhimu kwa kila mwananchi kuepuka kusajili laini kwa kuweka alama ya kidole zaidi ya mara moja ili kuzuia usajili wa laini nyingine za ziada ambazo zinaweza kutumika kufanya uhalifu mitandaoni

“Wananchi wengi wamekuwa wahanga wa utapeli mitandaoni hivyo Wizara imejipanga kuimarisha mifumo ya kulinda faragha na taarifa binafsi ili zisitumike vibaya na watu wasiokuwa na nia njema”, alizungumza Dkt. Ndugulile

Aidha, amewaasa wananchi kuacha kutoa taarifa binafsi au kufuata maelekezo yeyote kwa watu wanaopiga simu na kujitambulisha wanatoka dawati la huduma kwa mteja katika makampuni ya simu ili kuepuka kutapeliwa

Ameongeza kuwa namba wanayotakiwa kupigiwa na makampuni ya simu ni namba 100 na sio kupigiwa na namba kutoka mitandao tofauti na mitandao wanayotumia huku wakijitambulisha wametoka huduma kwamteja na kuomba taarifa zao za kifedha au kutaka kujua salio lililopo katika laini zao za simu.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari




Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Wananchi Wasisitizwa Kufanya Uhakiki Wa Laini Za Simu
Wananchi Wasisitizwa Kufanya Uhakiki Wa Laini Za Simu
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi_Mx1BeeDE67xWayOoLMat1N5MNxe2s8A5PDd0gY0GQnKvKGQ6oHfKeknxbo9y-frB9JdcsUkB8Y6xN5965dqFARmsR5W_USzR8I-b1fX402AC5mEG8N6mN9fZDfz6TJXuTGN5iikzP4RN/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi_Mx1BeeDE67xWayOoLMat1N5MNxe2s8A5PDd0gY0GQnKvKGQ6oHfKeknxbo9y-frB9JdcsUkB8Y6xN5965dqFARmsR5W_USzR8I-b1fX402AC5mEG8N6mN9fZDfz6TJXuTGN5iikzP4RN/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/wananchi-wasisitizwa-kufanya-uhakiki-wa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/wananchi-wasisitizwa-kufanya-uhakiki-wa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy