BAADA ya Ofisa wa Habari wa Simba, Haji Sunday Manara, kuweka hadharani chuki anazodaiwa kufanyiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa timu ...
BAADA ya Ofisa wa Habari wa Simba, Haji
Sunday Manara, kuweka hadharani chuki
anazodaiwa kufanyiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu
(CEO) wa timu hiyo, Barbara Gonzalez,
hatimaye uongozi wa Simba umetoa tamko.
Sauti iliyosambaa mitandaoni ambayo inadaiwa
ni ya Manara, ilisikika ikisema:“Barbara una chuki mbaya sana kwangu hadi naogopa kula mbele yako, naacha hii timu kwa ajili yako kwa sababu ya chuki yako kwangu, unajiona wewe ni Simba kuliko wote, unataka umaarufu kinguvu.
“Unadhalilisha wafanyakazi wa Simba na
kuwatishia, unatamani kuniondoa Simba,
sitakubali na hujui lolote kuhusu hii klabu,
subiri hii mechi ipite.
“Nasingiziwa eti nilienda Kigamboni kwenye
kambi ya Yanga, vitu vya hovyo kabisa, mimi
sinunuliki kwa thamani ya fedha Barbara
kwangu haya ni matusi.”
Baada ya maneno hayo kuzuka, Championi
lilimtafuta mwenyekiti wa Simba, Murtaza
Mangungu, ili azungumzie ishu hiyo ambapo
alisema: “Tunasubiri mechi ya Kigoma iishe ndipo
tuweze kuongea nao na kutatua tatizo ila kwa
sasa tumeweka akili zetu kwenye mchezo wa
Kigoma.
“Suala la wao kwenda Kigoma au kutokwenda
waulize wenyewe watakujibu.”
Jumapili hii Simba itakuwa ikicheza na Yanga
kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho kule
Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS