MZEE MPILI:TUTAWAFUNGA SIMBA MAGOLI YA KUHESABU KIGOMA
HomeMichezo

MZEE MPILI:TUTAWAFUNGA SIMBA MAGOLI YA KUHESABU KIGOMA

  SHABIKI na Mwanachama maarufu wa Klabu ya Yanga mzee Haji Mpili ameweka wazi kuwa ushindi wa bao 1-0, walioupata dhidi ya Simba, Julai 3...

WAWILI WA YANGA KUIKOSA NAMUNGO, YUPO MTAMBO WA MABAO PIA
YALIYOPITA SI NDWELE, WAWAKILISHI WETU GANGENI YAJAYO
HIZI HAPA PIA MBALI YA DABI RATIBA ILIBADILIKA, ILA GOMA LILIPIGWA

 SHABIKI na Mwanachama maarufu wa Klabu ya Yanga mzee Haji Mpili ameweka wazi kuwa ushindi wa bao 1-0, walioupata dhidi ya Simba, Julai 3, 2021 yeye ndio alicheza mchezo huo na kuhakikisha Simba haishindi.

 

Mzee Mpili ambaye alionekana na baadhi ya viongozi wa juu wa Yanga siku kadhaa kabla ya mechi amesema alichokifanya kwa Mkapa ni siri yake na atakifanya tena kwenye mechi ya fainali ya Kombe la Azam Federatio kati ya Yanga na Simba, itakayochezwa katika Uwaja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, Julai 25, 2021.

 

“Hii ya tarehe 3 ilikuwa salamu tu derby yenyewe ni tarehe 25 Kigoma kwa sababu Simba wana kelele sana na kelele zao tunajua akina nani wanawapa hizo kelele, mimi ndo nilikuwa mchezaji namba moja wa ule mpira na Kigoma ndo utachezwa mpira wa uhakika.

 

“Mchezo wa Kigoma nimeshamaliza kazi, Kigoma hawatoki ng’ooo, niache kama nilivyo hawatoki. Wapeni habari kwamba Mzee Mpili amesema kama alivyowafungeni Dar es Salaam na Kigoma mtafungwa, tena magoli ya Kigoma ni ya kuhesabu.

 

"Nilijua tutashinda, hata kama Simba angetangulia kufunga ningesawazisha na kuongeza goli la pili. Tunajua Simba inajipanga kulipa kisasi kwenye mchezo wa Fainali ya FA lakini tayari wamechelewa Kigoma wanakufa tena na shughuli imeisha, tunawapiga tena.

 

“Nimepewa guarantee asilimia 100 kuwa mechi ya Kigoma imeisha na tutashinda goli mbili kwenda mbele. Kama wanasema Jumamosi tulibahatisha sawa. Lakini Shughuli yote wataiona kigoma, hatuwezi kuliacha hilo Kombe,” amesema Mzee Mpili ambaye kwa sasa ana-trendi mitandaoni kila kukicha.

 

Yanga inasubiri kukutana na Simba kwa mara ya nne kabla ya kukamilisha msimu huu huku ikiweka rekodi ya kutokufungwa na Simba kwenye michezo mitatu mfululizo.


Kwenye ligi ilikuwa mechi mbili ambapo ile ya awali ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 1-1 Simba, ule wa pili ulisoma Simba 0-1 Yanga na wa awali ilikuwa ni Kombe la Mapinduzi, Zanzibar, Yanga ilishinda kwa penalti 4-3.



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: MZEE MPILI:TUTAWAFUNGA SIMBA MAGOLI YA KUHESABU KIGOMA
MZEE MPILI:TUTAWAFUNGA SIMBA MAGOLI YA KUHESABU KIGOMA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjU3TguJI9Nv7a4Adf0SsCVaJ5xTm7V4Yd1eUByYtWdud5N0H5JC07FaNqjBYtIaSzVga1JBCyJFMeTUX4FfMr_2lWotp5NqNj7Vf2NP-mALb_kjp7pBHLwocJ-Ip-7P2VV_JKUK8VqFe7Q/w640-h406/Mpili+wasafi.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjU3TguJI9Nv7a4Adf0SsCVaJ5xTm7V4Yd1eUByYtWdud5N0H5JC07FaNqjBYtIaSzVga1JBCyJFMeTUX4FfMr_2lWotp5NqNj7Vf2NP-mALb_kjp7pBHLwocJ-Ip-7P2VV_JKUK8VqFe7Q/s72-w640-c-h406/Mpili+wasafi.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/mzee-mpilitutawafunga-simba-magoli-ya.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/mzee-mpilitutawafunga-simba-magoli-ya.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy