KWA SURA MPYA YANGA , KUNA JAMBO LINAKUJA
HomeMichezo

KWA SURA MPYA YANGA , KUNA JAMBO LINAKUJA

  S URA mpya za  viongozi wa Baraza  la Wadhamini wa  Klabu ya Yanga  ni ishara tosha  wamedhamiria kufanya  vema katika msimu ujao  ikiwe...

EURO 2020 KUKARIBISHWA NA MECHI KALI ZA KIMATAIFA
VIDEO: YANGA YAIPIGA BAO SIMBA ISHU YA MORRISON, SABABU YA CARLINHOS KUONDOKA
KIBURI KILICHOWAPONZA SIMBA, KITAWAMALIZA COASTAL UNION

 SURA mpya za viongozi wa Baraza la Wadhamini wa Klabu ya Yanga ni ishara tosha wamedhamiria kufanya vema katika msimu ujao ikiwemo kutwaa makombe.

 

Baraza hilo jipya linaundwa sura mpya tatu kati ya hao watano kati ya hao wanajua vizuri fitna za soka ndani na nje ya uwanja, hiyo huenda ikawa na faida kubwa kwao katika msimu ujao.

 

Tofauti na kuzijua fitna, pia wadhamini hao wana nafasi kubwa za uongozi Serikalini katika uongozi. Mwenyekiti wa Yanga, Dk Mshindo Msolla ndiye aliwatangaza wadhamini hao katika mkutano wake mkuu walioufanya wiki mbili zilizopita kwenye Ukumbi wa DYCCC, Changombe jijini Dar es Salaam.

 

Wadhamini wanaoongozwa na Dk Mwigulu Nchemba ambaye ni Waziri wa Fedha na Mipango aliyepewa nafasi hiyo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu.

Nchemba ndiye aliyefanikisha usajili wa kiungo mkabaji Salum Abdallah â€˜Fei Toto’ akiwa anaichezea Singida United ambayo alikuwa anaimiliki waziri huyo iliyokuwa inashiriki Ligi Kuu Bara.

 


Waziri huyo alipambana kuzima jaribio la watani wa Simba waliokuwa kwenye vita kubwa ya kumsajili kiungo huyo.

 

Mwingine ni Abbas Tarimba ambaye Mbunge wa Kinondoni, Dar pia aliwahi kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, hivyo analifahamu vizuri soka la hapa nchini.

 

Geoffrey Mwambe yeye ni Waziri wa Uwekezaji, kwa kupitia nafasi yake aliyokuwa nayo atasaidia timu hiyo katika mambo mbalimbali ili kufanikisha malengo yao ya kuchukua makombe.

 

Pia yupo Waziri wa Ofisi ya Rais Kazi Maalum, Kepteni George Mkuchika ambaye amekuwa katika kamati mbalimbali za Yanga kwa kipindi kirefu huku akiipambania katika mambo mbalimbali.


Na Mama Fatma Karume ambaye mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, yeye amekuwa akiipambania Yanga kwa muda mrefu katika kufikia mafanikio yao na ni mtu mwenye ushawishi mkubwa.

 

Mara kadhaa amekuwa akiisaidia na timu hiyo kila inapokwenda Unguja, Zanzibar kushiriki Kombe la Mapinduzi ambalo mwaka huu Yanga wamelichukua kwa kuwafunga Simba.Yupo aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Imani Madega ambaye yeye hayupo kwenye Baraza hilo, alikuwepo kwenye kamati iliyopitisha katiba mpya ya Mfumo wa Mabadiliko wa klabu hiyo.



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: KWA SURA MPYA YANGA , KUNA JAMBO LINAKUJA
KWA SURA MPYA YANGA , KUNA JAMBO LINAKUJA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiudxyAF9mxsCbkFmles4UO2G6JnAVXm9ad2wF41N9yPzAD_4jBB8YU83wL8Z_z_7eO0Rp-WPPMjqHg53atbT86BZTNnHCOiu6dAQ0AMltoliSc7nvuoxndr_27g5cBNH5w0uyVefmGIblM/w532-h640/Fei+mkataba.PNG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiudxyAF9mxsCbkFmles4UO2G6JnAVXm9ad2wF41N9yPzAD_4jBB8YU83wL8Z_z_7eO0Rp-WPPMjqHg53atbT86BZTNnHCOiu6dAQ0AMltoliSc7nvuoxndr_27g5cBNH5w0uyVefmGIblM/s72-w532-c-h640/Fei+mkataba.PNG
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/kwa-sura-mpya-yanga-kuna-jambo-linakuja.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/kwa-sura-mpya-yanga-kuna-jambo-linakuja.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy