MWAMUZI wa mtanange wa Yanga dhidi ya Simba kwenye mchezo wa fainali ya michuano ya Shirikisho la Azam (ASFC), Ahmed Arajiga, ameche...
MWAMUZI wa mtanange wa Yanga dhidi ya
Simba kwenye mchezo wa fainali ya michuano
ya Shirikisho la Azam (ASFC), Ahmed Arajiga,
amechezesha michezo miwili ya Simba ambayo
yote wameshinda na kufikia hatua ya fainali.
Timu hizo zinatarajia kushuka dimbani
leo Jumapili kwenye Uwanja wa Lake
Tanganyika, Kigoma ukiwa ni mchezo wa
kumtafuta bingwa wa michuano ya ASFC.
Takwimu zinaonyesha kuwa mwamuzi, Arajiga
ni faida kwa Simba ambapo kwenye michezo
miwili ya ASFC aliyochezesha ambayo ni ya
Robo fainali na Nusu fainali, Simba
wameshinda.
Mchezo wa kwanza ulikuwa dhidi ya Dodoma
Jiji uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini
Dar ambapo Simba waliibuka na ushindi wa
mabao 3-0, mchezo uliopigwa Mei 26, mwaka
huu.
Mchezo wa pili ulikuwa dhidi ya Azam FC,
uliopigwa Juni 26, mwaka huu kwenye Uwanja
wa Majimaji, Songea ambapo Simba iliibuka na
ushindi wa bao 1-0.
Mwamuzi huyo mwenyeji wa mkoani Manyara
hajachezesha mchezo wowote wa Yanga kwenye michuano ya Shirikisho la Azam kwa
msimu huu.
Kuhusu suala la mwamuzi huyo, Yanga waliandika maoni kwamba uteuzi wa mwamuzi huyo wanaona kama hawajauelewa kwa kuwa amechezesha mechi nyingi za wapinzani wao.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi Tanzania, Sud Abdi alitoa taarifa kwamba sababu mojawapo inayofanya waweze kumteua mwamuzi ni pamoja na mechi ambazo amechezesha uwezo wake pamoja na vigezo vingine ambavyo wanazingatia.
Hata Ulaya amebainisha kuwa huwa wanafanya hivyo kwa kumchukua mwamuzi kulingana na mashindano amechezesha katika mashindano husika.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS