BAO LA MAUYA LAMTESA GOMES, AJUTIA MUDA ALIOTUMIA KUWAFUATILIA
HomeMichezo

BAO LA MAUYA LAMTESA GOMES, AJUTIA MUDA ALIOTUMIA KUWAFUATILIA

  KOCHA Mkuu wa Simba, Mfaransa, Didier Gomes, amesema anasikitika muda mwingi aliopoteza kutazama video za michezo iliyopita ya watani w...

 


KOCHA Mkuu wa Simba, Mfaransa, Didier Gomes, amesema anasikitika muda mwingi aliopoteza kutazama video za michezo iliyopita ya watani wao wa jadi, Yanga na mwishoni mwa siku wakapoteza dhidi yao.


Jumamosi,Julai 3 Simba ikiwa mwenyeji wa mchezo huo wa Ligi Kuu Bara, ilijikuta ikifungwa 1-0 na Yanga kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, huku mfungaji akiwa Zawadi Mauya dakika ya 11.


Kipigo hicho kimevuruga mipango ya Simba ya kutwaa taji la Ligi Kuu Bara mbele ya Yanga kwani wangeshinda, basi wangetangaza ubingwa mbele ya watani wao wa jadi.


 Akizungumza na Spoti Xtra, Gomes alisema kabla ya mchezo huo, alitenga muda mwingi kwa ajili ya kuangalia mbinu na aina ya uchezaji wanayotumia Yanga, hivyo ameumia kupata matokeo hayo mabaya.


Gomes alisema baada ya kupoteza mchezo huo, hivi sasa wanaweka nguvu katika michezo ya ligi iliyosalia dhidi ya Coastal Union, Azam FC na Namungo FC.



“Bado mchezo wetu wa dabi unaniuma sana baada ya matokeo mabaya tuliyoyapata, na kama kocha mimi ndiye ninayewajibika katika hili, nafahamu mashabiki wameumia sana.


“Mechi hii ilikuwa na umuhimu mkubwa kwetu, siyo jambo zuri kupoteza mechi kubwa ya namna hii ambayo ndani yake ilikuwa na rekodi nyingi bora kama tungepata ushindi.



“Baada ya kupoteza, nguvu zangu nazielekeza katika michezo ya ligi iliyo mbele yetu,” alisema Gomes.


Wakati Gomes akisema hivyo, mfungaji wa bao hilo, Mauya alisema: “Kiukweli hatukuwa na presha kwenye mechi yetu na Simba ndiyo maana tumeshinda huku tukicheza vizuri.


“Tulifanya majukumu yaleyale ambayo tunayafanya kwenye mechi nyingine na mazoezini na tuliendelea kucheza kwa kujiamini. Tunaenda kufanya hivi tena Kigoma," .



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: BAO LA MAUYA LAMTESA GOMES, AJUTIA MUDA ALIOTUMIA KUWAFUATILIA
BAO LA MAUYA LAMTESA GOMES, AJUTIA MUDA ALIOTUMIA KUWAFUATILIA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjEQ4-znqu9_SQ-qbLVhjAHVKoVHFuDV7Si0JDx3WmWHUK8wNd5SshCkf6Rup4Xy11MXkB8acTuEwJQJF8AIcAzd2p0y3Pb-0pYSs3LZ97-4neMkopSH85gPvA2lp8iqC8GFRti8slX0b2p/w640-h426/simbasctanzania-210534455_844777113081546_359669230042643953_n.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjEQ4-znqu9_SQ-qbLVhjAHVKoVHFuDV7Si0JDx3WmWHUK8wNd5SshCkf6Rup4Xy11MXkB8acTuEwJQJF8AIcAzd2p0y3Pb-0pYSs3LZ97-4neMkopSH85gPvA2lp8iqC8GFRti8slX0b2p/s72-w640-c-h426/simbasctanzania-210534455_844777113081546_359669230042643953_n.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/bao-la-mauya-lamtesa-gomes-ajutia-muda.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/bao-la-mauya-lamtesa-gomes-ajutia-muda.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy