HITIMANA Thiery, raia wa Rwanda amewapa tahadhari Yanga kucheza kwa umakini mechi zao zilizobaki kwa kuwa wakiteleza kidogo watawapa naf...
HITIMANA Thiery, raia wa Rwanda amewapa tahadhari Yanga kucheza kwa umakini mechi zao zilizobaki kwa kuwa wakiteleza kidogo watawapa nafasi kubwa wapinzani wao Simba kutwaa ubingwa mapema.
Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 67 inafuatiwa na Yanga iliyo nafasi ya pili na pointi 61 huku Azam FC ikiwa nafasi ya tatu na pointi 60.
Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery ambaye aliwahi kuzifundisha timu za Namungo na Mtibwa Sugar alisema kuwa mzigo walionao Yanga ni mzito wakiteleza kidogo wanapeleka ubingwa mikononi mwa Simba.
Thiery amesema:-“Ukitazama Yanga na Simba wote wanahitaji ubingwa lakini bado Simba ana nafasi kubwa ya kuongoza kutokana na mechi alizonazo mkononi ila itakuwa kazi nyepesi kwake kushinda ikiwa Yanga atashindwa kupata matokeo.
“Kwa namna yoyote ile ninavyojua ni kwamba baada ya Simba kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika nguvu zao ni kwenye ligi unadhani nini kitatokea? Hapo ni lazima wapinzani wao kucheza kwa juhudi na umakini.
"Ushindani ni mkubwa na ligi inaonekana kuwa ngumu hivyo ni lazima kila timu kufanya vizuri kupata matokeo," .
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS