KIUNGO mkabaji wa Simba, Jomas Mkude amemuaga mshikaji wake Francis Kahata ambaye ameaga rasmi kwa mashabiki na viongozi wake kwa muda ...
KIUNGO mkabaji wa Simba, Jomas Mkude amemuaga mshikaji wake Francis Kahata ambaye ameaga rasmi kwa mashabiki na viongozi wake kwa muda ambao alikuwa ndani ya kikosi.
Kahata amekuwa mchezaji wa kwanza kuaga Simba baada ya kandarasi yake ya miaka miwili kumeguka ndani ya kikosi hicho.
Jana nyota huyo aliwaaga mashabiki na wachezaji wenzake kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kueleza kuwa anakwenda kuanza changamoto mpya.
Mkude amesema kuwa ni wakati mgumu ila lazima ufike kwa kuwa ni hatua ya maisha lakini atamkumbuka Kahata.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS