Kauli ya Rais Samia juu Katiba Mpya na mikutano ya hadhara
HomeHabari

Kauli ya Rais Samia juu Katiba Mpya na mikutano ya hadhara

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kumpa muda aimarishe uchumi wa nchi ili aweze kuangalia suala la Katiba Mpya n...

Habari Zilizopo katika Magazeti ya leo Disemba 20
Maafisa, Askari 14 Wa Tawa Wavishwa Vyeo Vipya Vya Jeshi La Uhifadhimaafisa, Askari 14 Wa Tawa Wavishwa Vyeo Vipya Vya Jeshi La Uhifadhi
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Disemba 19


Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kumpa muda aimarishe uchumi wa nchi ili aweze kuangalia suala la Katiba Mpya na mikutano ya hadhara ambayo kwa sasa imezuiwa.

Ameeleza hayo  jana Jumatatu Juni 28, 2021 wakati akijibu maswali mbalimbali ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini aliokutana nao Ikulu jijini Dar es Salaam,  yakiwemo ya mchakato wa Katiba Mpya na kuzuiwa kwa mikutano hiyo.

“Kama inavyosemwa nimeanza vizuri naomba nipeni muda nisimamishe nchi kwanza kiuchumi. Tuite wawekezaji wawekeze ajira zipatikane uchumi ufunguke halafu tutashughulikia Katiba, tutashughulikia mikutano ya hadhara wakati ukifika.

“Kwa sasa tunaruhusu mikutano ya ndani ya vyama  na wabunge wapo huru kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo yao si maeneo ya wengine..., ile yeyeee ingieni..., hili naomba sana Watanzania tujipe muda tufanye uchumi wetu..., sisemi katiba si ya maana lakini naomba mnipe muda kwanza nisimamishe uchumi kisha tutatizama mengine,” alisema Samia.

Alisema katika hotuba yake bungeni hivi karibuni alieleza atakutana na viongozi wa vyama vya siasa ili kujadili mustakabali wa siasa na Taifa.

“Sasa hivi nchi yetu ina changamoto nyingi sana, kuna janga la corona, uchumi umeshuka tunatakiwa kuupandisha. Na hili nataka niliunganishe na lile la Katiba Mpya. Kuna mambo mengi ya kushughulikia, nimesema ninakwenda kuifungua nchi kwa sababu uchumi umeshuka tunatakiwa kupandisha uchumi, tukifungua nchi.”

“Kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji kazi ambayo tumeifanya vizuri sana nataka niwaambie wawekezaji waliosajiliwa kipindi cha Machi hadi Mei mwaka huu ni mara mbili ya waliosajiliwa mwaka jana kipindi kama hiki,” alisema Samia.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Kauli ya Rais Samia juu Katiba Mpya na mikutano ya hadhara
Kauli ya Rais Samia juu Katiba Mpya na mikutano ya hadhara
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg7JgdJu9vPUS6YYX3rRiCkF9N3lvnraF0bwOEQ432GBtRcZmQn0NB-kQF9_xUSRXfdhl-6HLZNTNLmpfpdGsCwGQ_24mMEkoGT-aewi1PViEpYotX8-X0LldbSnc0Dj7hlTZ_DzY1TyI56/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg7JgdJu9vPUS6YYX3rRiCkF9N3lvnraF0bwOEQ432GBtRcZmQn0NB-kQF9_xUSRXfdhl-6HLZNTNLmpfpdGsCwGQ_24mMEkoGT-aewi1PViEpYotX8-X0LldbSnc0Dj7hlTZ_DzY1TyI56/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/06/kauli-ya-rais-samia-juu-katiba-mpya-na.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/06/kauli-ya-rais-samia-juu-katiba-mpya-na.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy