ISHU YA MANJI KUIBUKIA KWENYE MKUTANO WA YANGA IPO HIVI
HomeMichezo

ISHU YA MANJI KUIBUKIA KWENYE MKUTANO WA YANGA IPO HIVI

  K WA kiasi fulani, taarifa  za aliyekuwa Mwenyekiti  wa Yanga, Yusuf Manji,  kukosekana katika Mkutano  Mkuu wa klabu hiyo uliopangwa  ...

 


KWA kiasi fulani, taarifa za aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, kukosekana katika Mkutano Mkuu wa klabu hiyo uliopangwa kufanyika Jumapili hii, zinaweza kuwa mbaya kwa wapenzi na wanachama wa klabu hiyo.

 

Hatua hiyo inakuja baada ya Manji kurejea nchini hivi karibuni na kuleta matumaini kwa Wanayanga waliotarajia kumuona katika mkutano huo uliopangwa kufanyika Ukumbi DYCCC, Chang’ombe, Dar.

 

Yanga katika mkutano huo miongoni mwa ajenda zake zitakuwa ni mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo kwenda katika mfumo wa kisasa.Hivi karibuni, ziliibuka taarifa za Manji kulipia kadi ya uanachama ya klabu hiyo ambayo ingemruhusu kushiriki mkutano mkuu, lakini watu wake wa karibu, wamekanusha uwepo wa taarifa hizo.

 

Mtu wa karibu na Manji, amelithibitishia Spoti Xtra kwamba, kigogo huyo ataondoka nchini kabla ya kufanyika kwa mkutano huo, huku akiweka wazi kwamba, kiongozi huyo hakulipia kadi yake ya uanachama tangu atue nchini.

 

“Manji hakulipia ile kadi ya uanachama kama ambavyo watu wanasema, mwenyewe kabla ya mkutano mkuu kufanyika, atakuwa ameshaondoka hapa nchini, hivyo ni ngumu sana kwake kuwepo siku hiyo,” alisema mtu huyo.

 

Taarifa za Manji kukosekana katika mkutano huo, zitawashtua Wanayanga ambao wamekuwa na mapenzi makubwa na kiongozi wao huyo wa zamani ambaye hivi karibuni alirejea nchini baada ya kuondoka kwa muda mrefu kwani walipanga kumjadili kurudi kwake.

 

Manji aliwahi kuwa kiongozi wa Yanga kwa takribani miaka saba kuanzia 2012 hadi 2017 ambapo aliifanya timu hiyo kuwa tishio akifanikisha kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara tatu mfululizo kuanzia 2014 hadi 2016.



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: ISHU YA MANJI KUIBUKIA KWENYE MKUTANO WA YANGA IPO HIVI
ISHU YA MANJI KUIBUKIA KWENYE MKUTANO WA YANGA IPO HIVI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhkteJcLXc9Lo3Iwh7fjceIUa8DzNHI_iR4_fytK-L9kpSW-QVG7RZGlDcGT8nehSJWeNAECxfGONP9RSkgU3LFKUGVAbz3FKiRZjCteYHOD8VjOnZVzs-IMhH_Xk7RZphyKtX9N_fn-YNh/w640-h392/Manji.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhkteJcLXc9Lo3Iwh7fjceIUa8DzNHI_iR4_fytK-L9kpSW-QVG7RZGlDcGT8nehSJWeNAECxfGONP9RSkgU3LFKUGVAbz3FKiRZjCteYHOD8VjOnZVzs-IMhH_Xk7RZphyKtX9N_fn-YNh/s72-w640-c-h392/Manji.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/06/ishu-ya-manji-kuibukia-kwenye-mkutano.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/06/ishu-ya-manji-kuibukia-kwenye-mkutano.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy