HALMASHAURI ya Buchosa, Mkoa wa Mwanza imefanikiwa kushika nafasi ya pili katika mashindano ya michezo shule za msingi ngazi ya mkoa yal...
HALMASHAURI ya Buchosa, Mkoa wa Mwanza imefanikiwa kushika nafasi ya pili katika mashindano ya michezo shule za msingi ngazi ya mkoa yaliyoshirikisha halmashauri saba zinazounda mkoa huo.
Halmashauri hizo ni Nyamagana, llemela, Magu, Kwimba, Buchosa, Sengerema na Misungwi zilizoshirikisha jumla ya wanafunzi wanamichezo 800.
Halmashauri ya Buchosa imeshika nafasi ya pili kwa ushindi wa jumla kwa kupata makombe nane katika michezo yote iliyoshiriki huku kinara wa michezo hiyo ikiwa ni Halmashauri ya Magu iliyobeba makombe 12 kwenye mashindano hayo.
Aidha, halmashauri ya Buchosa imetoa wanafunzi 12 wanamichezo katika michezo mbalimbali kuunda timu ya mkoa wa Mwanza ambayo itakuwa na jumla ya wanamichezo 100 watakaoshiriki mashindano ya UMITASHUMTA kitaifa yatakayofanyika mkoani Mbeya mwaka huu.
Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Eric Shigongo anawatakia kila laheri vijana wa Buchosa waliofanikiwa kuchaguliwa kuunda timu ya UMITASHUMTA mkoa wa Mwanza na timu yote ya mkoa huo, wakapambane Kitaifa na kupata mataji mengi zaidi.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS