BAADA ya dakika 90 kukamilika na ubao wa Uwanja wa FNB Soccer City kusoma Kaizer Chiefs 4-0 Simba, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ...
BAADA ya dakika 90 kukamilika na ubao wa Uwanja wa FNB Soccer City kusoma Kaizer Chiefs 4-0 Simba, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa walicheza hovyo.
Kichapo hicho kinakuwa cha kwanza kwa Kocha Mkuu Didier Gomes kushuhudia idadi kubwa ya mabao kwa timu yake ikifungwa akiwa katika benchi baada ya kupokea mikoba ya Sven Vandenbroeck.
Haji Manara kupitia Ukurasa wake wa Istagram alisema:" Alhamdulillah. Tumefungwa na aliye bora usiku wa leo, tumecheza hovyo na tumefanya makosa mengi yaliyostahili adhabu hii.
"Life go on na still tunazo dk tisini nyingine za kuamua,".
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS