MKUDE RUKSA KUJIUNGA YANGA, MKATABA WAKE SIMBA BADO
HomeMichezo

MKUDE RUKSA KUJIUNGA YANGA, MKATABA WAKE SIMBA BADO

  U NAAMBIWA huko Simba,  Jonas Mkude, mambo  yake yanazidi kumwendea  kombo baada ya kuwepo  kwa taarifa za chini kwa chini kuwa,  Mwenye...


 UNAAMBIWA huko Simba, Jonas Mkude, mambo yake yanazidi kumwendea kombo baada ya kuwepo kwa taarifa za chini kwa chini kuwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa timu hiyo, Mohamed Dewji ‘Mo’, amegomea suala la kumuongeza mkataba mpya.

 

Mkude ni miongoni mwa wachezaji wanaomaliza mkataba Simba mwishoni mwa msimu huu.

 

Hivi karibuni uongozi wa Simba, uliwatangaza baadhi ya nyota wake walioongeza mkataba mpya, ambapo walianza na Clautos Chama, kisha wakahamia kwa wazawa, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ na baadaye John Bocco na Shomari Kapombe.

 

Chanzo chetu makini kimeliambia Championi Ijumaa kuwa, kwa namna ambavyo Mkude ameendelea kuwa na matukio ya utovu wa nidhamu, uongozi wake umesita kumuongeza mkataba kiasi cha kuruhusu hata akitaka aende Yanga.

 

Mkude hajaonekana kwenye mechi mbili za Simba dhidi ya Dodoma Jiji na ile ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Kaizer Chiefs Jumamosi iliyopita, ikieleza kuwa ameomba ruhusa kutokana na matatizo binafsi.

 

Hata hivyo, duru za michezo zinadai kuwa Simba hawana mpango wa kumbakiza klabuni hapo.“Hivi unajua kama Mkude bado hajaongezewa mkataba mpya, na kwa jinsi ninavyoona sina uhakika kabisa kama ataongezewa maana uongozi hadi sasa umemchunia na uko tayari hata kumuona akisaini Yanga, maana wamechoshwa na matukio yake ya utovu wa nidhamu,” kilisema chanzo hicho.

 

Championi Ijumaa lilimtafuta Mkuu wa Maudhui wa Simba, Ally Shatry ‘Bob Chico’ ili kujua juu ya taarifa za mkataba wa Mkude, ambapo alisema: “Mkude bado yupo kikosini na atakuwa safarini kuelekea Ruangwa kwenye mchezo wetu na Namungo, hivyo taarifa za wachezaji kuongeza mkataba tayari tulishazitoa.

 

"Ila kuna baadhi yao bado tupo kwenye mazungumzo nao, hivyo kila atakayekuwa tayari ameongezewa mkataba nadhani tutaweka wazi ila kwa sasa kuhusu usajili naomba utambue hivyo tu.”



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: MKUDE RUKSA KUJIUNGA YANGA, MKATABA WAKE SIMBA BADO
MKUDE RUKSA KUJIUNGA YANGA, MKATABA WAKE SIMBA BADO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgVrtFWTSxxfKJtLRNgwZXgs7eC_180__-zRKy5DKJHJkUhnaxFvDtx4ttY8ylptBvgt9fdV9GrSiwE_2ASKvMP9CsXSgPaASxrEvj9S7XuymM5yedyuZe_leLJ1t9UCpEFaml0h3nfr76_/w640-h494/Mkude+rukwa.PNG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgVrtFWTSxxfKJtLRNgwZXgs7eC_180__-zRKy5DKJHJkUhnaxFvDtx4ttY8ylptBvgt9fdV9GrSiwE_2ASKvMP9CsXSgPaASxrEvj9S7XuymM5yedyuZe_leLJ1t9UCpEFaml0h3nfr76_/s72-w640-c-h494/Mkude+rukwa.PNG
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/05/mkude-ruksa-kujiunga-yanga-mkataba-wake.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/05/mkude-ruksa-kujiunga-yanga-mkataba-wake.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy