MCHEZO MZIMA KWA YANGA KUIMALIZA MWADUI FC ULICHEZWA HIVI
HomeMichezo

MCHEZO MZIMA KWA YANGA KUIMALIZA MWADUI FC ULICHEZWA HIVI

  KIRAKA wa Yanga, Deus Kaseke jana Uwanja wa Kambarage alitimiza majukumu yake kwa kupachika mabao mawili mbele ya Mwadui FC na kuwafanya...

CLATOUS CHAMA AFUNGUKA ISHU YA TUZO BONGO
YANGA YAINGIA ANGA ZA KIPA HUYU WA MALI
SIMBA YATUMIA MBINU ZA YANGA KUMNASA STRAIKA, NDANI YA CHAMPIONI JUMAMOSI

 KIRAKA wa Yanga, Deus Kaseke jana Uwanja wa Kambarage alitimiza majukumu yake kwa kupachika mabao mawili mbele ya Mwadui FC na kuwafanya wasonge mbele hatua ya nusu faiinali.

Chini ya Kocha Mkuu, Nassredine Nabi Yanga waliendeleza mwendo wa ushindi baada ya kutoka kushinda mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania kwenye mchezo wa ligi na jana ilikuwa ni Kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali.

Ushindi huo utaifanya timu hiyo kukutana na Biashara United ambayo ilishinda nayo mabao 2-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wao wa hatua ya robo fainali.

 Kaseke alianza kupachika bao la kwanza dakika ya 24 baada ya kipa namba moja wa Mwadui FC, Mussa Mbissa kufanya makosa akiwa na mpira ndani ya 18 ambao aliupoka kwa beki wake yeye mwenyewe.

 Kasi ilizidi kipindi cha kwanza ila Mwadui walikuwa imara na kuweza kwenda mapumziko ubao wa Uwanja wa Kambarage ukisoma Mwadui 0-1 Yanga.

Kipindi cha pili, Yanga walianza kwa kasi sawa na Mwadui na ni Yacouba Songne alimtengeneza pasi kiraka Kaseke ambaye hakuwa na ajizi alipachika bao la pili dakika ya 56.

Ingekuwa umakini wa Yanga wangefunga mabao mengi ila shukrani kwa kipa Mbissa ambaye dakika ya 54 aliokoa jaribio la Ditram Nchimbi, dakika ya 53 na 43 aliokoa hatari ya Yacouba na wote walifanya majaribio hayo ndani ya eneo la 18. Nje ya 18 lilikuwa ni jaribio la Kibwana Shomari.

Kaseke naye alikuwa na nafasi ya kufunga mapema dakika ya 10 ila mikono ya Mbissa iliokoa hatari hiyo na licha ya mpira kukutana na Yacouba naye alikosa kupachika bao hilo.

Ni Denis Richard alifanya jaribio moja dakika ya 49 kwa Farouk Shikalo ila liliokolewa , Wallace Kiango alifanya jaribio dakika ya 44, Salim Aziz dakika ya 64 akiwa nje ya 18 alifanya jaribio liliokolewa na Shikalo na kuwafanya washindwe kupata bao na kuaga mashindano hayo.



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: MCHEZO MZIMA KWA YANGA KUIMALIZA MWADUI FC ULICHEZWA HIVI
MCHEZO MZIMA KWA YANGA KUIMALIZA MWADUI FC ULICHEZWA HIVI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi7dlxRt7MjhBNxuTnOXlPpYILzUHve-lqEz6X1ogU9D5siWjJJu9YAPiuiQsLPpBT5zDvCa43XemtZKN95px5Zf4Skyl5DkxYOgyushG4aObHqc0FN4GwzwQn2R7wmIaT6nXZc3HmaECQh/w640-h640/yangasc-190934695_251068216763956_2456488623794682369_n.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi7dlxRt7MjhBNxuTnOXlPpYILzUHve-lqEz6X1ogU9D5siWjJJu9YAPiuiQsLPpBT5zDvCa43XemtZKN95px5Zf4Skyl5DkxYOgyushG4aObHqc0FN4GwzwQn2R7wmIaT6nXZc3HmaECQh/s72-w640-c-h640/yangasc-190934695_251068216763956_2456488623794682369_n.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/05/mchezo-mzima-kwa-yanga-kuimaliza-mwadui.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/05/mchezo-mzima-kwa-yanga-kuimaliza-mwadui.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy