Kongamano la Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kufanyika Mei 21, 2021
HomeHabari

Kongamano la Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kufanyika Mei 21, 2021

  Na Mwandishi Wetu, Dodoma Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo imeandaa Kongamano la Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika ikiw...

 


Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo imeandaa Kongamano la Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika ikiwa ni hatua ya kutambua mchango wa Tanzania katika Ukombozi wa Bara hilo ambalo litaambatana na Siku ya Uanuai wa Utamaduni Dunani.

Akizungumza katika mahojiano na kituo cha Redio cha Dodoma FM kupitia kipindi cha “Kapu Kubwa”, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni, Dkt. Emmanuel Temu ameelezea jinsi Wizara ilivyojipanga kufanikisha maadhimisho hayo ambayo yanatarajia kufanyika Mei 21, 2021 Jijini Dar es Salaam.

"Maadhimisho haya yameanza kufanywa kidunia tangu mwaka 2001 ambapo mwaka huu Wizara kupitia Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika imeandaa kongamano litakalokusanya fikra za wanamajumui wa Afrika kujadili kwa kina mchango wa Tanzania kwenye Ukombozi wa Bara la hili" amesema Dkt.Temu.

Dkt.Temu amefafanua kuwa kongamano hilo linaloongozwa na kaulimbiu ya “Urithi wa Ukombozi Fahari ya Afrika” ni fursa muhimu ya kuwaleta pamoja wanazuoni na wadau wote wa utamaduni kujadili mustakabali wa  harakati hizo ili kuendelea kuhifadhi historia ya harakati hizo kwa faida ya vizazi vya sasa na  baadae.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo nchini, Yusufu Singo alipofanya mahojiano na Kituo cha Redio cha A FM cha Jijini Dodoma amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Vyombo vya Habari ili kunogesha Michezo hapa nchini.

“Habari na Michezo ni Sekta zinazotegemeana  sana  kwa  mfano mwisho wa juma hili  tuna mechi ya Simba na Yanga, bila  umma kuelezwa vizuri juu ya mechi hii inaweza kukosa msisimko” amesisitiza  Mkurugenzi Singo.

Pamoja na kongamano hilo pia kutakuwa na kikao kazi cha Maafisa Utamaduni na Maafisa Michezo wote nchini kinachoandaliwa na kuratibiwa na Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo kitakachofanyika kuanzia Mei 21 hadi 23, 2021 kitakachofanyika Jijini Dar es salaam.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Kongamano la Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kufanyika Mei 21, 2021
Kongamano la Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kufanyika Mei 21, 2021
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiVP6CnHzmIH2FVZlyCyZfD5_fPfUmlBFsqksJEEl_6YChFuzSVd19Ed4Z7KJtuT4uJgDYambTzunB1Drk8y-k7CcQFvq25Ziy8Yww-fIaVMI-I3p-ZyLFUzFpjY-ew6CVEepfIR1Kuze2p/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiVP6CnHzmIH2FVZlyCyZfD5_fPfUmlBFsqksJEEl_6YChFuzSVd19Ed4Z7KJtuT4uJgDYambTzunB1Drk8y-k7CcQFvq25Ziy8Yww-fIaVMI-I3p-ZyLFUzFpjY-ew6CVEepfIR1Kuze2p/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/05/kongamano-la-urithi-wa-ukombozi-wa-bara.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/05/kongamano-la-urithi-wa-ukombozi-wa-bara.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy