Fidia Uwanja Wa Ndege Msalato Na Barabara Ya Mzunguko Kulipwa Hivi Karibuni
HomeHabari

Fidia Uwanja Wa Ndege Msalato Na Barabara Ya Mzunguko Kulipwa Hivi Karibuni

Serikali imesema kuwa itaanza zoezi la ulipaji fidia hivi karibuni kwa  wananchi wote waliochukuliwa maeneo yao ili kupisha miradi ya kim...

Viwanja Vinauzwa Kigamboni Gezaulole Kwa Bei Nzuri Kabisa
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo May 12
VIDEO: Rosa Ree – It’s Your Birthday


Serikali imesema kuwa itaanza zoezi la ulipaji fidia hivi karibuni kwa  wananchi wote waliochukuliwa maeneo yao ili kupisha miradi ya kimkakati ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato na barabara ya mzunguko ya jiji la Dodoma kwa njia nne (Km 112.3).

Aidha imeelezwa kuwa kiasi cha Shilingi Bilioni 12.7 imeshatolewa na kupelekwa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa ajili ya fidia za mradi wa ujenzi wa barabara ya mzunguko ya jiji la Dodoma na kiasi cha shilingi Bilioni 14.5 kwa ajili ya malipo ya fidia kwa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa
Msalato.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Msalato na Matumbulu jijini Dodoma, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho, amesema kuwa fidia hiyo italipwa kwa kuzingatia sheria na kusisitiza kuwa kila anayedai fidia hiyo atalipwa fedha yake yote.

“Leo nimekuja hapa kuwaeleza kuwa msiwe na wasiwasi juu ya fidia zenu, fedha zimepatikana na mtalipwa kwa mujibu wa sheria zote za nchi zilizopo, pia malalamiko yatasikilizwa kwa wale ambao hawataridhika”, amesema Waziri Chamuriho.

Dkt. Chamuriho amewaelezea wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuwa barabara hiyo itajengwa kwa sehemu mbili ambapo sehemu ya kwanza itahusisha Nala – Veyula – Mtumba – Ihumwa Dry Port (Km 52.3) na sehemu ya pili itaanzia Ihumwa Dry Port – Matumbulu – Nala (Km 60) na tayari wakandarasi wa ujenzi wa sehemu hizo wameshapatikana.  

Amebainisha kuwa miradi hiyo ikikamilika itasaidia kuvutia fursa za uwekezaji  na hivyo kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa jiji la Dodoma na Taifa kwa ujumla.

Amewataka wananchi wa maeneo yanayopitiwa na miradi hiyo kutoa ushirikiano ili kurahisisha zoezi la ulipaji fidia kufanyika kama lilivyopangwa ili miradi hiyo ya kimkakati kuanza mapema na kukamilika kwa wakati.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Selemani Kakoso, ameitaka Wizara kusimamia wakanadarasi hao kikamilifu katika miradi hiyo na kuhakikisha kuwa inakamilika kwa wakati kwa mujibu wa mikataba iliyowekwa.

Ametoa wito kwa wananchi wanaopitiwa na miradi hiyo kuhakikisha kuwa wanatoa ushirikiano kwa makandarasi na kuacha          tabia ya kuhujumu miundombinu ili kupelekea miradi kukamilika kwa wakati.

Awali akitoa taarifa kwa Kamati, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale, ameeleza kuwa mradi wa ujenzi wa barabara ya mzunguko utahusisha pia ujenzi wa miradi mingine inayohusisha jamii moja kwa moja ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya vinne, visima vya maji vinne na magari matano ya kubebea wagonjwa.

Naye Mbunge wa Dodoma Mjini, Mheshimiwa Anthony Mavunde, ameishukuru Serikali kwa kuamua kuanza utekelezaji wa miradi hiyo hivi karibuni kwani kukamilika kwa miradi hiyo kutapelekea kuchangamsha na kuleta maendeleo katika jiji la Dodoma.

Miradi ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya mzunguko ya Dodoma (Km 112.3) kwa njia nne na Uwanja wa Ndege wa Msalato inafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa fedha za mkopo nafuu  kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Fidia Uwanja Wa Ndege Msalato Na Barabara Ya Mzunguko Kulipwa Hivi Karibuni
Fidia Uwanja Wa Ndege Msalato Na Barabara Ya Mzunguko Kulipwa Hivi Karibuni
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhFjrHdr_0FnIT7rkAqszvCu5wN5JZ_kmLCu-dzEs5AW-bLgeeS0BWGJVQsBrePhA0izxKhPmA3RpyHt9LwzEE6B7GxIPD1kaLH4nWEi_Fmpo7p8jVK_rcc2PvhvC52P2Bk8AH8gIt96ws1/s16000/1.jpeg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhFjrHdr_0FnIT7rkAqszvCu5wN5JZ_kmLCu-dzEs5AW-bLgeeS0BWGJVQsBrePhA0izxKhPmA3RpyHt9LwzEE6B7GxIPD1kaLH4nWEi_Fmpo7p8jVK_rcc2PvhvC52P2Bk8AH8gIt96ws1/s72-c/1.jpeg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/05/fidia-uwanja-wa-ndege-msalato-na.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/05/fidia-uwanja-wa-ndege-msalato-na.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy