YANGA YAWAPIGA MKWARA WAZEE WA PIRA GWARIDE, MASHINE ZAO ZA KAZI HIZI HAPA
HomeMichezo

YANGA YAWAPIGA MKWARA WAZEE WA PIRA GWARIDE, MASHINE ZAO ZA KAZI HIZI HAPA

 UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa una imani ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa kesho Aprili 30, mbele ya Tanzania Prisons wenye sera ya ...


 UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa una imani ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa kesho Aprili 30, mbele ya Tanzania Prisons wenye sera ya pira gwaride ambao ni wa Kombe la Shirikisho.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi umeweka kambi kwa muda Mbeya kabla ya kuibukia Songea kwa ajili ya mchezo huo wa hatua ya 16 bora.

Kikosi hicho kilitinga hatua hiyo kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ken Gold katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru na bao pekee la ushindi lilifungwa kwa mkwaju wa penalti na Fiston Abdulazack ambaye kwa sasa yupo na kikosi pia.

Nyota wengine ambao wapo kwenye msafara huo ni pamoja na Ramadhan Kabwili, Farouk Shikahlo na Metacha Mnata kwa upande wa makipa.

Dickson Job na Abdala Shaibu, 'Ninja' kwa upande wa mabeki pamoja na Paul Godfrey, 'Boxer'.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wanatambua Tanzania Prisons ni timu ngumu na imara ila watapambana kupata matokeo.

"Katika hali ya kawaida, Tanzania Prisons ni timu imara na inafanya vizuri kwenye mechi zake zote na hata tukikutana nao huwa inakuwa ngumu kupata matokeo ila haina maana kwamba hatuna uwezo wa kupata ushindi kwao.

"Kwa maandalizi ambayo tunayafanya imani yetu tunakwenda kufanya kweli na kutafuta ushindi, mashabiki waendelee kutupa sapoti uwezo na nia ipo," .

Mchezo wao wa kwanza Yanga kucheza Uwanja wa Nelson Mandela ulikuwa ni wa ligi na walilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 hata ule wa mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Yanga 1-1 Prisons.



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: YANGA YAWAPIGA MKWARA WAZEE WA PIRA GWARIDE, MASHINE ZAO ZA KAZI HIZI HAPA
YANGA YAWAPIGA MKWARA WAZEE WA PIRA GWARIDE, MASHINE ZAO ZA KAZI HIZI HAPA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgXNgBzZu435ux2w3pQ-BuiJQAgZYXNbf-w6RcWCDisq9u3V5BNqz3pQ3hEE2vcrx6Ssb1g3IkZI4u6bWzkdJwTMRJFows8v2WqC2o1sONxZoCoUhMNSm3w0-U1nf0gnGohMpDDN4BokajS/w506-h640/Job+Mbeya.PNG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgXNgBzZu435ux2w3pQ-BuiJQAgZYXNbf-w6RcWCDisq9u3V5BNqz3pQ3hEE2vcrx6Ssb1g3IkZI4u6bWzkdJwTMRJFows8v2WqC2o1sONxZoCoUhMNSm3w0-U1nf0gnGohMpDDN4BokajS/s72-w506-c-h640/Job+Mbeya.PNG
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/04/yanga-yawapiga-mkwara-wazee-wa-pira.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/04/yanga-yawapiga-mkwara-wazee-wa-pira.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy