WASHAMBULIAJI WA SIMBA, MUGALU NA BOCCO WAPEWA PROGRAM MAALUMU KUIMALIZA AS VITA
HomeMichezo

WASHAMBULIAJI WA SIMBA, MUGALU NA BOCCO WAPEWA PROGRAM MAALUMU KUIMALIZA AS VITA

KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes amewaandalia programu maalumu washambuliaji wake Chris Mugalu, John Bocco kwa ajili ya kuwaongezea makal...


KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes amewaandalia programu maalumu washambuliaji wake Chris Mugalu, John Bocco kwa ajili ya kuwaongezea makali ili waweze kucheka na nyavu. 

 Simba inatarajiwa kuvaana na AS Vita katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa kesho, Aprili 2 Jumamosi saa kumi kamili kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Bocco na Mugalu walipewa program maalum ya jinsi ya kufunga mabao pekee muda mfupi baada ya kumalizika kwa mazoezi ya jumla ya kikosi cha timu hiyo.

 

Katika mazoezi hayo yaliyofanyika Simba Mo Arena, Bunju, Dar, saa kumi kamili jioni, kocha huyo alimtaka kila mshambuliaji apige shuti au kumchambua huku akiwatengea kila mmoja mipira kumi kwa ajili ya kupiga golini na kufunga.

 

Gomes aliwatengea mipira hiyo nje ya 18 na kuwataka kupiga golini kwa ajili ya kufunga na lengo likiwa ni kuwaongezea umakini wanapofika katika eneo la hatari la wapinzani wakiwa katika maandalizi ya mchezo dhidi ya AS Vita.

 

Kocha huyo alitumia program hiyo kwa zaidi ya dakika 15 kwa kila mmoja kupiga mashuti 10 kwa kubadilishana huku golikipa akiwa Beno Kakolanya.Program hiyo iliwataka mastaa hao kupiga mashuti kwa kubadilisha miguu, kulia na kushoto, kabla ya baadaye kuwaongezea program ya kupiga mipira kwa kichwa.

 

Mipira hiyo ya vichwa ilikuwa inapigwa kutokea pembeni na kiungo mshambuliaji raia wa Kenya, Francis Kahata ambayo kati ya hiyo Bocco alifunga bao moja, huku mingine tisa ikiishia mikononi mwa Kakolanya.

 

Kwa upande wa Mugalu, hakufanikiwa kufunga.Akizungumzia kuhusu safu yake ya ushambuliaji, Gomes amesema: “Safu yangu ya ulinzi imekuwa ikifanya vizuri sana lakini safu yangu ya ushambuliaji imekuwa inashindwa kutumia kwa ufasaha nafasi tunazotengeneza, jambo ambalo ni lazima tulifanyie kazi.


“Mchezo wetu dhidi ya AS Vita ni muhimu kupata ushindi mzuri wa mbao mengi tukiwa katika uwanja wa nyumbani, kikubwa tunataka kumaliza tukiwa kileleni katika kundi letu.”



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: WASHAMBULIAJI WA SIMBA, MUGALU NA BOCCO WAPEWA PROGRAM MAALUMU KUIMALIZA AS VITA
WASHAMBULIAJI WA SIMBA, MUGALU NA BOCCO WAPEWA PROGRAM MAALUMU KUIMALIZA AS VITA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj0IWstvVLhAjPOCcOjU2rE9qXc59ja4Ix48r4Kfs0KCwkwv9cMaxZCAOPrKlC9dZ4m9gsEfyhXbjL88eTzIsuY3sXEbt2FAjK7rspAXi1G9WMRUL2ROgvDxQceRj9bhL_MdyZnvTpkPiM8/w640-h360/Mugalu+v+As+Vita.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj0IWstvVLhAjPOCcOjU2rE9qXc59ja4Ix48r4Kfs0KCwkwv9cMaxZCAOPrKlC9dZ4m9gsEfyhXbjL88eTzIsuY3sXEbt2FAjK7rspAXi1G9WMRUL2ROgvDxQceRj9bhL_MdyZnvTpkPiM8/s72-w640-c-h360/Mugalu+v+As+Vita.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/04/washambuliaji-wa-simba-mugalu-na-bocco.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/04/washambuliaji-wa-simba-mugalu-na-bocco.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy