BEKI wa kati wa Klabu ya Simba, Joash Onyango leo Aprili 5 amekabidhiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki wa mwezi Machi (Emirate Alum...
BEKI wa kati wa Klabu ya Simba, Joash Onyango leo Aprili 5 amekabidhiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki wa mwezi Machi (Emirate Aluminium Simba Fans Player of the Month)
Onyango alikuwa anashindana kupata tuzo na mshindi wa Mwezi Februari, kiungo Luis Miquissone ambaye alikuwa ameingia kwa mara nyingine tena kwenye mchakato wa kuisaka tuzo hiyo kwa mwezi Machi.
Pia nyota mwingine ambaye alikuwa kwenye mchakato wa kuwania tuzo hiyo ni kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula.
Baada ya kura kupigwa kupitia mtandao ambapo mashabiki ni wapigaji wa kura hizo wamempa ushindi beki wao Onyango ambaye leo amekabidhiwa tuzo yake.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS