KOCHA Mkuu wa Simba, Mfaransa Didier Gomes amegoma kuona mastaa wake wakiondoka kwenye kikosi chake katika msimu ujao. Kati ya masta...
KOCHA Mkuu wa Simba, Mfaransa Didier Gomes amegoma kuona mastaa wake wakiondoka kwenye kikosi chake katika msimu ujao.
Kati ya mastaa wanaotajwa kuondoka Simba ni Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jr’ anayedaiwa kusaini mkataba wa awali Yanga, Joash Onyango kwenda Orlando Pirates na Aishi Manula kuwaniwa na Mamelodi Sundowns zote za Afrika Kusini.
Zimbe Jr au Tshabalala hivi sasa anaelekea kuwa mchezaji huru kwa kuwa mkataba wake unaelekea mwishoni.
“Muda wa usajili bado lakini nimeona vema
kulizungumzia hili la wachezaji wangu
wanaodaiwa kuondoka Simba mwishoni
mwa msimu huu baada ya mikataba yao
kumalizika.
“Binafsi sitakubali kuona wachezaji wangu hao wakiondoka kutokana na umuhimu mkubwa waliokuwa nao katika timu, kwani siku zote ni hatari kwa timu kufanya mabadiliko ya kikosi kwa kuwaondoa wachezaji walioipa mafanikio timu hasa msimu huu kimataifa.
“Lakini kingine sifahamu kuhusu kuondoka
kwao, kitu kikubwa nitakachoweza kusema
kuwa natamani kubakia na wote katika
misimu mingine miwili hadi mitatu katika
kutengeneza timu bora kwa ajili ya
mafanikio ya timu, ” alisema Gomes.
Chanzo:Championi
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS