Bunge Lapitisha Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 hadi 2025/26.
HomeHabari

Bunge Lapitisha Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 hadi 2025/26.

 Na. Farida Ramadhani na Peter Haule, WFM, Dodoma Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania  Jumatatu tarehe 12 Aprili, 2021 limepitisha M...

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo March 21
Makombora Ya Urusi Yaipiga Shule Walikohifadhiwa Watu 400
Urusi yadai kuwauwa wanajeshi 100 wa Ukraine mjini Schytomyr


 Na. Farida Ramadhani na Peter Haule, WFM, Dodoma
Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania  Jumatatu tarehe 12 Aprili, 2021 limepitisha Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22  hadi 2025/26.

Mpango huo utakaogharimu zaidi ya shilingi trilioni 114.8 umepangwa kutekeleza maeneo makuu matano ya kipaumbele, ikiwemo kuchochea uchumi shindani na shirikishi, kuimarisha uwezo wa uzalishaji viwandani na utoaji huduma.

Vipaumbele vingine ni kukuza uwekezaji na biashara, kuchochea maendeleo ya watu na kuendeleza rasilimali watu.

" Tutahakikisha kwamba miradi yote ya kimkakati iliyoainishwa kwenye Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa  Miaka Mitano itatekelezwa kama ilivyopangwa", alisema Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) wakati akihitimisha mjadala kuhusu Mpango huo Bungeni jijini Dodoma.


Shabaha ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 hadi 2025/26 ni pamoja na kupandisha kiwango cha ukuaji wa uchumi kutoka asilimia 6.0 ya mwaka 2021 hadi kufikia wastani wa asilimia 8.0 itakapofika mwaka 2026.

Aidha mfumuko wa bei umebashiriwa kuendelea kubaki katika wigo wa tarakimu moja kwa wastani wa asilimia kati ya 3.0 hadi 5.0 katika kipindi cha muda wa kati na akiba za kigeni kukidhi mahitaji ya uagizaji wa huduma na bidhaa kutoka nje kwa kipindi kisichopungua miezi minne.

Malengo mengine ni kuhakikisha kuwa mapato ya ndani ikijumuisha mapato ya Halmashauri yanaongezeka kutoka asilimia 15.9 ya pato la Taifa mwaka 2021/22 hadi asilimia 16.8 itakapofika mwaka 2026 na sekta binafsi inatarajiwa kuzalisha ajira mpya zipatazo milioni nane kati ya Julai 2021 na Juni 2026.

Miongoni mwa viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango, waliohudhuria uhitimishaji wa mjadala huo wakiongozwa na Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) ni  Naibu wake Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) pamoja na Manaibu Katibu Mkuu  Bi. Amina Khamis Shaaban na Bw. Adolf Ndunguru na baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Bunge Lapitisha Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 hadi 2025/26.
Bunge Lapitisha Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 hadi 2025/26.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEivZiz8aYWUkrmReXF3FeCru3hpj-ztz7GSr767kyDzwVtAsGLvjnnoPPrOGMrEfMvdK-D5f0CSWl0WdQ_zEJXI1YmkLhQRc4raaxVjbXqutK9_xTHo49reoG7ZKIyM69rfcceWgPNeQzRK/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEivZiz8aYWUkrmReXF3FeCru3hpj-ztz7GSr767kyDzwVtAsGLvjnnoPPrOGMrEfMvdK-D5f0CSWl0WdQ_zEJXI1YmkLhQRc4raaxVjbXqutK9_xTHo49reoG7ZKIyM69rfcceWgPNeQzRK/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/04/bunge-lapitisha-mpango-wa-tatu-wa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/04/bunge-lapitisha-mpango-wa-tatu-wa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy