Tume Ya Haki Za Binadamu Na Utawala Bora Yakutana Na Wadau Jijini Dodoma Kujadili Taarifa Ya Mapendelkezo 227 Yaliyotolewa Na Baraza La Haki Za Binadamu Duniani
HomeHabari

Tume Ya Haki Za Binadamu Na Utawala Bora Yakutana Na Wadau Jijini Dodoma Kujadili Taarifa Ya Mapendelkezo 227 Yaliyotolewa Na Baraza La Haki Za Binadamu Duniani

 Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma TUME ya Haki za Binadamu na utawala bora nchini imekutana  na wadau  wa Idara,Taasisi na Wizara mbalim...

Habari Zilizopo katika Magazeti ya Leo Novemba 6
Taarifa Kwa Umma Kuhusu Kurejesha Mfumo Wa Tarura Wa Ulipaji Wa Ushuru Wa Maegesho Ya Vyombo Vya Usafiri Wa Njia Ya Kielektroniki
Rais Samia Afungua Kongamano La Kumbukizi Ya Historia Ya Maalim Seif Sharif Hamad


 Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
TUME ya Haki za Binadamu na utawala bora nchini imekutana  na wadau  wa Idara,Taasisi na Wizara mbalimbali za Serikali Jijini Dodoma kwa lengo la kujadili taarifa ya mapendekezo  zaidi ya  227  yaliyotolewa na Baraza la haki za Binadamu Duniani kuhusiana na maendeleo ya masuala ya haki za binadamu.

Akizungumza katika kikao cha kujadili taarifa hiyo,Mwenyekiti wa Tume hiyo,Jaji mstaafu Mathew Mwaimu amesema kuwa Tanzania kama nchi mwanachama wa Baraza hilo la haki za binadamu hutakiwa kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa kama ushauri  kuhusiana na masuala ya maendeleo ya haki za binadamu.

Jaji Mwaimu amesema kuwa kutokana na mapendekezo hayo  ambayo yapo 227 yaliyotolewa na Baraza hilo la haki za binadamu  kwa  Tanzania kama mwanachama ambayo iliyakataa baadhi ya mapendekezo takribani 93 yalitolewa na Baraza hilo mwaka 2016.

 Amesema kila baada ya miaka minne wamekuwa wakituma taarifa ya maendeleo ya haki za binadamu ambapo ifikapo Machi25 mwaka huu Tanzania itapeleka taarifa hiyo makao makuu ya Baraza la haki za binadamu nchini Geneva Uswiss.

 Amesema maeneneo mengine ambayo hawajayaweka katika taarifa hiyo ambayo ina kurasa tano watachagua yale ya muhimu na kupokea ushauri na kuyaboresha mapendekezo hayo.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo,Muhamed Hamisi Hamad amesema kuwa taarifa hiyo ya haki za binadamu inahusu Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na wamechukua hatua mbalimbali zimefanyika ikiwemo haki za wanawake ikiwemo uteuzi wa nafasi za wanawake katika uongozi

 Naye Kamishina paul Masanja wa Tume ya haki za binadamu na utawala bora amesema kuwa Tanzania kama mwanachama wa umoja wa mataifa na wadau wa haki za binadamu wanawajibika kutoa ripoti kwa Baraza hilo ili kuonyesha kama hayo yanafanyika nchini

Kuna masuala mbalimbali ya haki za kijamii na kiuchumi zimefikiwa ikiwemo maji,afya kwa makundi mbalimbali ambapo utekelezaji wake umepiga hatua.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Tume Ya Haki Za Binadamu Na Utawala Bora Yakutana Na Wadau Jijini Dodoma Kujadili Taarifa Ya Mapendelkezo 227 Yaliyotolewa Na Baraza La Haki Za Binadamu Duniani
Tume Ya Haki Za Binadamu Na Utawala Bora Yakutana Na Wadau Jijini Dodoma Kujadili Taarifa Ya Mapendelkezo 227 Yaliyotolewa Na Baraza La Haki Za Binadamu Duniani
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjWrJBj5DhTMF99aEn2lIsa4vexy2bXIXN6jkYpb4kzpmDgbigptqlnHr_oZeLXyf0556jGUMb1cqCBwd-jN4xWVLIXKAKxyuVs2p88gX2IGORIITi8txTes0YKshmpO6JJMVm620wiDE6I/s16000/1.png
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjWrJBj5DhTMF99aEn2lIsa4vexy2bXIXN6jkYpb4kzpmDgbigptqlnHr_oZeLXyf0556jGUMb1cqCBwd-jN4xWVLIXKAKxyuVs2p88gX2IGORIITi8txTes0YKshmpO6JJMVm620wiDE6I/s72-c/1.png
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/03/tume-ya-haki-za-binadamu-na-utawala.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/03/tume-ya-haki-za-binadamu-na-utawala.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy