IKIWA inaongoza Ligi ya Wanawake Tanzania, Klabu ya Simba Queens imeweka rekodi yake ndani ya dakika 1,350 kwa kucheza bila kufungwa. S...
IKIWA inaongoza Ligi ya Wanawake Tanzania, Klabu ya Simba Queens imeweka rekodi yake ndani ya dakika 1,350 kwa kucheza bila kufungwa.
Simba Queens ambao ni mabingwa watetezi wamecheza jumla ya mechi 15 na hawajaonja joto ya kupoteza mchezo.
Ni mechi 3 walilazimisha sare huku wakishinda 12 wamekusanya pointi 39 huku watani zao wa jadi, Yanga Princes wakiwa nafasi ya pili na pointi 38 ila wamepoteza mchezo mmoja.
Kocha wa Simba Queens, Mussa Mgosi amesema kuwa wachezaji wanajituma na kufanya majukumu ambayo wamepewa.
"Wachezaji wanajituma uwanjani ili kutimiza majukumu yao kwani wanatambua ili kupata ushindi ni lazima kufunga ukizingatia kwamba sisi ni mabingwa watetezi.
"Msimu huu ushindani umekuwa tofauti hilo linatupa nguvu ya sisi kuzidi kufanya vizuri kwenye mechi zetu zijazo," .
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS