KUMBE YANGA WALIWAPIGA BAO KAIZER CHIEFS KWA KISINDA NA MUKOKO
HomeMichezo

KUMBE YANGA WALIWAPIGA BAO KAIZER CHIEFS KWA KISINDA NA MUKOKO

  VIUNGO tegemeo hivi sasa ndani ya Yanga, Wakongomani Mukoko Tonombe na Tuisila Kisinda, wamemshawishi Skauti Mkuu wa Klabu ya Kaizer Ch...

 


VIUNGO tegemeo hivi sasa ndani ya Yanga, Wakongomani Mukoko Tonombe na Tuisila Kisinda, wamemshawishi Skauti Mkuu wa Klabu ya Kaizer Chiefs ya nchini Afrika Kusini, Walter Steenbok kwenda kutembelea ofisi za klabu hiyo.

 

Tofauti na skauti huyo, viongozi wengine waliofika kutembelea ofisi hizo mpya zilizopo Mtaa wa Samora, Posta jijini Dar es Salaam ni Siyabulela Loyilane naye kutoka Afria Kusini, Rudolfs kutoka Latvia na Andrew kutoka Uganda waliojulikana kwa jina moja moja.

 

Tonombe na Tuisila ni kati ya wachezaji tegemeo katika kikosi cha Yanga waliojiunga nayo msimu huu wakitokea AS Vita ya Kinshasa, Congo.


 Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassani Bumbuli alisema skauti alishawishika kuja kuitembelea Yanga baada ya kupata taarifa za wachezaji Tonombe na Tuisila kujiunga na klabu hiyo katika msimu huu.

 

Bumbuli alisema kuwa skauti huyo alipewa kazi ya kuwafuatilia viungo hao mwaka jana na mabosi wakubwa wa Kaizer Chiefs kwa kutakiwa kwenda Congo kuwatazama, lakini alipofika akapata taarifa za nyota hao kujiunga na Yanga.

 

Aliongeza kuwa baada ya kupata taarifa hizo haraka alirejea nyumbani kwao Sauzi kwa ajili ya kurudisha majibu ya taarifa za nyota hao, hivyo alipofika nchini katika Kongamano la Wanamichezo lililofanyika juzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akaomba kwenda kuitembelea klabu hiyo ya Yanga ili kujua ukubwa na jinsi wanavyojiendesha.

 

“Juzi tulipokea ugeni mkubwa kutoka kwa viongozi mbalimbali wa soka nchini lakini hasa kwa Skauti Mkuu wa Kaizer Chiefs ambaye ni Steenbok aliyeomba kuja kutembelea ofisi zetu na kikubwa kujionea jinsi klabu inavyojiendesha.

 

“Na kikubwa zaidi walitaka kufahamu tuliwezaje kuwaona na kuwasajili akina Tonombe na Tuisila, hivyo mara baada ya kufika ofisini walikutana na Kaimu Katibu Mkuu Mfikirwa (Haji), Mshauri wa Klabu, Senzo (Mazingisa) na Injinia (Hersi Said).


“Katika kikao walishauriana mambo mengi ya kuhusu klabu hizi mbili za Kaizer Chiefs na Yanga.

 

“Skauti huyo alielezea mipango yao waliyonayo Kaizer Chiefs ya kuwasajili Tonombe na Tuisila kabla ya sisi kuwasajili kuja kuichezea Yanga, kiukweli alionekana kusikitika kuwakosa wachezaji hao,” alisema Bumbuli.


Chanzo:Championi



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: KUMBE YANGA WALIWAPIGA BAO KAIZER CHIEFS KWA KISINDA NA MUKOKO
KUMBE YANGA WALIWAPIGA BAO KAIZER CHIEFS KWA KISINDA NA MUKOKO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg7w-nRVWqw2h8EGFyt1hWVL4x2Kq_K2ILye6Wq1nS1ikGUArR20tk1cs3jX1IQF21zbFk_cjSHghfOiQCo2ktQ-5F-1ZGzut0kUNxsYwWoC-aEY7piP1b0loAUnChyqSkCow-Uh-xShIwf/w566-h640/Tonombe.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg7w-nRVWqw2h8EGFyt1hWVL4x2Kq_K2ILye6Wq1nS1ikGUArR20tk1cs3jX1IQF21zbFk_cjSHghfOiQCo2ktQ-5F-1ZGzut0kUNxsYwWoC-aEY7piP1b0loAUnChyqSkCow-Uh-xShIwf/s72-w566-c-h640/Tonombe.JPG
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/03/kumbe-yanga-waliwapiga-bao-kaizer.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/03/kumbe-yanga-waliwapiga-bao-kaizer.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy