GOMES ANAAMINI KWAMBA MANULA ATACHEZA MBELE YA AL MERRIKH
HomeMichezo

GOMES ANAAMINI KWAMBA MANULA ATACHEZA MBELE YA AL MERRIKH

KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa anaamini kipa wake namba moja Aishi Manula atakuwa sehemu ya kikosi kitakachowafuata Wasuda...


KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa anaamini kipa wake namba moja Aishi Manula atakuwa sehemu ya kikosi kitakachowafuata Wasudan, Al Merrikh ambao watacheza nao Machi 6, kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Manula aliumia jana Machi Mosi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania, dakika ya 67 wakati akiokoa mpira uliokuwa ukielekea langoni mwake baada ya kugongana na mshambuliaji Lyanga Daniel.

Gomes ambaye alikiongoza kikosi chake kushinda mabao 3-0 na kusepa na pointi tatu muhimu ameweka wazi kwamba kipa huyo ni muhimu ndani ya kikosi chake.

Dakika ambazo zilibaki langoni alikaa kipa namba mbili Beno Kakolanya ambaye aliendelea pale ambapo Manula ameishia kwa kuokoa hatari zilizokuwa zikienda langoni mwake.

"Baada ya mchezo kuisha daktari ameniambia kuwa kila kitu kipo sawa, amepelekwa hospitali ili kufanyiwa vipimo na tunasubiri majibu.

"Manula,(Aishi) ni mchezaji muhimu sana na nina uhakika ataweza kucheza Sudan,".

Ipo kundi A ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo imetinga hatua ya makundi na inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi sita.

Ina mtihani wa kusaka pointi tatu ugenini mbele ya Al Merrikh ambayo ina hasira kwa kupoteza mechi zake zote mbili ilizocheza.

Leo Machi 2 kikosi cha Simba kinatarajiwa kuanza safari kuelekea nchini Sudan kwa ajili ya mchezo huo muhimu ambao utakuwa na ushindani mkubwa ndani ya dakika 90.

Kwenye mechi zote za kimataifa kuanzia ile ya hatua ya awali dhidi ya FC Plateau ya Nigeria wakati Simba ikishinda kwa bao 1-0 ugenini na kwa Mkapa ngoma kuwa 0-0, Manula alikaa langoni.



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: GOMES ANAAMINI KWAMBA MANULA ATACHEZA MBELE YA AL MERRIKH
GOMES ANAAMINI KWAMBA MANULA ATACHEZA MBELE YA AL MERRIKH
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi8o9h1on7QXwbgTGZrIdD6rrVSoxZC8XmMCXj2e7H5XBorpsE8IOofn8KUAdBwTIBRa7AHcYDKo4We7KKQOc03TrIYnDtARlevuJ-sBW_qG2BUtSrOx16jCfwjjFPbMiK6J6pZORcMr0c4/w640-h426/Manula+Plateau.PNG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi8o9h1on7QXwbgTGZrIdD6rrVSoxZC8XmMCXj2e7H5XBorpsE8IOofn8KUAdBwTIBRa7AHcYDKo4We7KKQOc03TrIYnDtARlevuJ-sBW_qG2BUtSrOx16jCfwjjFPbMiK6J6pZORcMr0c4/s72-w640-c-h426/Manula+Plateau.PNG
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/03/gomes-anaamini-kwamba-manula-atacheza.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/03/gomes-anaamini-kwamba-manula-atacheza.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy