OFISA Habari wa zamani wa Klabu ya Yanga, Dismas Ten amesema kuwa kwake yeye ndani ya ardhi ya Tanzania Ofisa Habari bora kwenye vilabu...
OFISA Habari wa zamani wa Klabu ya Yanga, Dismas Ten amesema kuwa kwake yeye ndani ya ardhi ya Tanzania Ofisa Habari bora kwenye vilabu vya soka Tanzania ni Hassan Bumbuli wa Yanga na Idrissa Bandari wa Ndanda FC.
Ten amewahi kuwa Ofisa Habari wa Mbeya City na ndani ya Yanga amepitia nafasi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kaimu Katibu.
Kupitia Ukurasa wake wa Instagram amesema kuwa kuna tofaiyi kubwa kati ya Ofisa Habari na Msemaji hivyo kwake msemaji bora ni Haji Manara ambaye ni Ofisa Habari wa Simba.
"Linapokuja suala la kuongeza, kuzungumza hakuna kama Haji Manara yeye ni msemaji kweli.
"Ipo tofauti kati ya Ofisa Habari na msemaji,".
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS