CCM kuomboleza kwa siku 21 Kifo cha Rais Magufuli....kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kukutana Jumamosi
HomeHabari

CCM kuomboleza kwa siku 21 Kifo cha Rais Magufuli....kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kukutana Jumamosi

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza siku 21 za maombolezo, kufuatia kifo cha Mwenyekiti wa chama hicho Rais  Dkt John Magufuli.   Aki...


Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza siku 21 za maombolezo, kufuatia kifo cha Mwenyekiti wa chama hicho Rais  Dkt John Magufuli.

  Akizungumza na Waandishi wa habari jijini  Dodoma,  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, -Humphrey Polepole amesema  kuwa kufuatia msiba huo chama hicho kimesitisha shughuli zote za chama na bendera zitapeperushwa nusu mlingoti.

  Amesema viongozi wakuu wa CCM wa Tanzania Bara na Zanzibar wamekubaliana Kamati Kuu ikutane siku ya Jumamosi jijini Dar es salaam kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali.

  CCM imewaomba Wanachama wote wa chama hicho na watu wote wenye mapenzi mema na CCM pamoja na Watazania wote kusimama imara na kuendelea kutafakari mchango wa kihistoria wa Dkt Magufuli katika maendeleo ya Taifa.

“Ninawaletea taarifa ya msiba baada ya wakuu wa chama chetu kupokea tarifa rasmi, wakuu wa chama wametafakari baada ya hapo tunatoa taarifa ifuatayo;

“CCM kinatoa taarifa rasmi ya kifo cha Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambaye amekuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. CCM tumepikea kwa mshituko mkubwa taarifa za kifo cha mpendwa wetu Dkt. Magufuli.

“Taarifa ya serikali iliyotolewa na Makamu wa Rais, Mama Samia ilieleza kuwa ndugu Magufuli amefariki kwa tatizo la moyo, kitaalam cardio fibrillation. Wakuu wa chama waliopo wameshauriana na kukubaliana kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM taifa itaketi Jumamosi, Machi 20, 2021 ofisi ndogo ya CCM Lumumba Dar.

“Chama kitakuwa katika maombolezo ya siku 21 sambamba na tangazo za seerikali, bendera za chama zitapepea nusu mlingoti, kutakuwa na vitabu vya maombolezo bara na Zanzibar.

“Chama kinawaomba wananchama wote wa CCM na watu wote wenye mapenzi mema na nchi yetu kuwa na kuendelea kuwa watulivu huku tukitafakari mchango wa kipekee na kihistioria wa ndugu yetu ndugu Magufuli,” amesema Polepole.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: CCM kuomboleza kwa siku 21 Kifo cha Rais Magufuli....kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kukutana Jumamosi
CCM kuomboleza kwa siku 21 Kifo cha Rais Magufuli....kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kukutana Jumamosi
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEikXIz4Cmim9kCVBvq8t_NeFVfQYYpe1dmTyC_ofYdJtstiqKb3-fhvHMrINLOJmDjZ1t7IozN_ojUENxEx8EO5H8bFybyW6jGfmbAmiywAs78tYwccEiY7n1lHN5SCnj5HOvpYeRlqoXHk/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEikXIz4Cmim9kCVBvq8t_NeFVfQYYpe1dmTyC_ofYdJtstiqKb3-fhvHMrINLOJmDjZ1t7IozN_ojUENxEx8EO5H8bFybyW6jGfmbAmiywAs78tYwccEiY7n1lHN5SCnj5HOvpYeRlqoXHk/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/03/ccm-kuomboleza-kwa-siku-21-kifo-cha.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/03/ccm-kuomboleza-kwa-siku-21-kifo-cha.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy