Waziri Mkuu: Tuendelee Kumuomba Mungu Na Tuchukue Tahadhari
HomeHabari

Waziri Mkuu: Tuendelee Kumuomba Mungu Na Tuchukue Tahadhari

WAZIRI MKUU Kaasim Majaliwa amesema Watanzania wanaweza kuushinda ugonjwa wa corona kwa kumuomba Mungu na kufuata ushauri unaotolewa na ...


WAZIRI MKUU Kaasim Majaliwa amesema Watanzania wanaweza kuushinda ugonjwa wa corona kwa kumuomba Mungu na kufuata ushauri unaotolewa na wataalamu wa afya kuhusu njia za kujikinga na ugonjwa huo.

“Katika kipindi hiki ambacho dunia imekumbwa na wimbi la ugonjwa wa mlipuko, la muhimu kwetu ni kuendelea kumuomba Mungu kama Mheshimiwa Rais alivyotuasa tufunge kwa maombi ya siku tatu; Ijumaa kwa Waislamu kama walivyofanya, Jumamosi kwa Wasabato tumeona mwitikio wao na kwa Wakristo kesho Jumapili kama tulivyoona maandalizi yakifanyika,” amesema.

Akizungumza kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mazishi ya aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, (Jumamosi, Februari 20, 2021) Waziri Mkuu amesema: “Pamoja na kumuomba Mungu, ni lazima tuendelee kufuata maelekezo ya kitaalam ikiwemo kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka, tutumie vitakasa mikono na kuvaa barakoa.”

Kuhusu uvaaji wa barakoa, Waziri Mkuu amesema Serikali haijazuia mtu kujikinga lakini aliwataka wanaozitumia ni lazima wajiridhishe na ubora, usalama wake na wafahamu zimetoka wapi. “Ni lazima wanaozitumia wajue zimetoka wapi. Ni vema watu washone barakoa zao wenyewe au wanunue zilizotengenezwa na viwanda vya Tanzania kama alivyoshauri Rais wetu, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mwaka jana.”

Amesema: “Pamoja na maombi, Watanzania tunapaswa tuendelee kufuata maelekezo ya Serikali bila kuwa na hofu. Serikali kupitia maabara na vituo vya kutoa huduma, inaendelea kuhakikisha huduma zinapatikana 

Akimzungumzia marehemu Balozi Kijazi, Waziri Mkuu aliwapa pole wafiwa na wanafamilia kutokana na msiba huo mkubwa na akamuelezea kwamba, alikuwa kiongozi mwenye mapenzi mema na Taifa lake lakini pia alikuwa na uwezo wa kutoa ushauri ambao ulikuwa na manufaa kwa Taifa. “Tunalo jukumu la kumuenzi kwa kuendeleza na kutenda mema yote aliyotuachia.”

Ibada ya kumuombea Marehemu Balozi Kijazi ilifanyika katika kanisa la Mt. Agustino, eneo la Manundu, mjini Korogwe, mkoani Tanga na iliongozwa na Askofu Mstaafu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphory Mkude.

Mapema, akizungumza katika mazishi hayo, Mkuu wa Majeshi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo alisema wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama walikuwa karibu naye kwa sababu Balozi Kijazi alikuwa ni Katibu wa Baraza la Usalama la Taifa.

“Alikuwa ni mahiri, mpole na mwenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja ambazo zilieleweka na kukubalika katika vikao vyao,” alisema.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Bw. Martine Shigela alisema Balozi Kijazi alikuwa ni Baba, kiongozi na mwalimu na wakati wote alikuwa ni kielelezo cha uchapakazi na uadilifu kwa watu wa mkoa wa Tanga. “Na kwa sababu hiyo, mkoa umeamua kuwa stendi ya mabasi ya mji wa Korogwe itaitwa jina la Balozi John Kijazi kwa heshima yake na ili kutunza kumbukumbu yake,” aliongeza.

Mazishi hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri, makatibu wakuu na Wabunge wa mkoa wa Tanga.

Mhandisi Balozi Kijazi alizaliwa mkoani Mwanza akiwa ni mtoto wa pili kwenye familia ya watoto 10. Ameacha mke, watoto watatu pamoja na wajukuu wawili.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Waziri Mkuu: Tuendelee Kumuomba Mungu Na Tuchukue Tahadhari
Waziri Mkuu: Tuendelee Kumuomba Mungu Na Tuchukue Tahadhari
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgUc7PvXligCmFIQ9TB6QkLAWOk_3xai2WDDjGXvtuvq368k5dB_aFjCEtiOP3bn20Zw95qFjq-0xt-pgkgE0UPQ0cCcgPW_v-CRyVslp37t9aReMiq_DFZIoCqLpHCOXb69eyh8jLC8scY/s16000/2bd845fe-e4ce-4507-ae79-24a390b3a4b5.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgUc7PvXligCmFIQ9TB6QkLAWOk_3xai2WDDjGXvtuvq368k5dB_aFjCEtiOP3bn20Zw95qFjq-0xt-pgkgE0UPQ0cCcgPW_v-CRyVslp37t9aReMiq_DFZIoCqLpHCOXb69eyh8jLC8scY/s72-c/2bd845fe-e4ce-4507-ae79-24a390b3a4b5.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/02/waziri-mkuu-tuendelee-kumuomba-mungu-na.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/02/waziri-mkuu-tuendelee-kumuomba-mungu-na.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy