Wakazi Wa Kaliua Waishukuru Serikali Kwa Kuwapa Bilioni 3.3 Kwa Ajili Aya Miradi Ya Maendeleo
HomeHabari

Wakazi Wa Kaliua Waishukuru Serikali Kwa Kuwapa Bilioni 3.3 Kwa Ajili Aya Miradi Ya Maendeleo

NA TIGANYA VINCENT WAKAZI wa Wilaya ya Kaliua wameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwapelekea kiasi cha shilingi bilioni 3.3 kwa ...


NA TIGANYA VINCENT
WAKAZI wa Wilaya ya Kaliua wameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwapelekea kiasi cha shilingi bilioni 3.3 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya afya na elimu.

Fedha hizo zilitolewa Desemba ni kwa ajili ya uendelezaji wa ujenzi wa majengo katika Hospitali ya Wilaya, kusadia sekta ya elimu ya msingi na Sekondari na kusaidia mpango wa kunusuru kaya maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF).

Taarifa hiyo ilitolewa jana na  Mbunge wa Jimbo la Kaliua Aloyce Kwezi wakati mkutano na wazee kwa lengo la kuwashukuru kwa kumchagua yeye kuwa Mwakilisha wao Bungeni na kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa ajili kuwaongoza tena kipindi kingine.

Alisema kupatikana kwa fedha hizo kutawasaidia kuharakisha kukamilika kwa Hospitali ya Wilaya na kuwawezesha kupata huduma katika mazingira yao.

Kwezi aliongeza kuwa Hospitali hiyo ni muhimu kwao kwa kuwa itasaidia kuwaondolea adha ambazo wakinamama wajawazito walikuwa wakizipata ikiwemo kutozwa fedha kwa ajili ya glovu wanapokwenda kujifunga na kutozwa gharama kubwa wanapohitaji damu na wazee kuambaiwa kuwa hakuna dawa wanapokwenda kutibiwa katika Hospitali binafsi.

Katika kutekeleza ahadi mbalimbali alizotoa ,Kwezi alisema kwa upande wake ameshatoa kiasi cha shilingi milioni 70  kutoka Mfuko wa Jimbo ambazo amezipeleka katika Kata zote wa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo ya wananchi.

Alisema ataendelea kukutana mara kwa mara na wananchi kusilikiza kero na matatizo yao mbalimbali na kuyatafutia ufumbi ili yasije yakawa kiwazo katika maendeleo yao.

Kwezi alisema katika kipindi alichokutana na kundi la wazee amebaini kuwepo kwa kero nyingi ikiwemo wazee kukosa dawa wanapokwenda kutibiwa , wakimama wajawazito kuamuliwa kununua vitu ambavyo havipo katika miongozo ya Wizara ya afya na ndugu wa wagonjwa kutozwa kiasi kingi cha chupa za damu kuliko anachohitaji mgonjwa.

Alisema anapanga kukutana na Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji kwa ajili ya kupanga mpango wa kuwaandaa wataalamu ili waweze kujibu na kutafutia ufumbuzi chamngamoto hizo kwa wakati.

Aidha Mbunge huyo aliishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuanzisha mradi wa upelekaji maji ya ziwa Victoria kupitia Urambo.

Alisema tayari wataalamu wameshafika wilayani humo na wakati wowote utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo utaanza na kuongeza kuwa kukamilika kwa mradi kutaongeza fursa za uwekezaji katika sekta ya kilimo na ufugaji

Katika hatua nyingine Kwezi alisema ataendelea kuhamasisha suala na michezo katika vijiji na mashule kwa lengo la kuibua vipaji.

Alisema hatua hiyo itasaidia vijana wengi kupata fursa za ajira kupitia sekta hiyo na kuitangaza vema Wilaya ya Kaliua ndani na nje ya Tanzania.

Kwezi alisema hadi hivi sasa ameshakwisha kutoa vifaa mbalimbali vya michezo kwa vijiji vyote vya Jimbo lake na awamu inafuata ni kupeleka mashuleni.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Wakazi Wa Kaliua Waishukuru Serikali Kwa Kuwapa Bilioni 3.3 Kwa Ajili Aya Miradi Ya Maendeleo
Wakazi Wa Kaliua Waishukuru Serikali Kwa Kuwapa Bilioni 3.3 Kwa Ajili Aya Miradi Ya Maendeleo
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi2eEdsNUkfo4e_N89zHh-HSCEKTOvXCrJ-IV-ZVSjBwhJYR0IlbVkF9a1a-BuzAZyQo8NdC8xQv5JxvoZLWXpQ-aPjhg3wEZU0lQ5UGFhcLRZBfMImIY4kOL3MiiGUsXjdwOnJsmgZ5hyr/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi2eEdsNUkfo4e_N89zHh-HSCEKTOvXCrJ-IV-ZVSjBwhJYR0IlbVkF9a1a-BuzAZyQo8NdC8xQv5JxvoZLWXpQ-aPjhg3wEZU0lQ5UGFhcLRZBfMImIY4kOL3MiiGUsXjdwOnJsmgZ5hyr/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/02/wakazi-wa-kaliua-waishukuru-serikali.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/02/wakazi-wa-kaliua-waishukuru-serikali.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy