Serikali Yaanzisha Kitengo Cha Miliki Kutatua Migogoro Ya Ardhi
HomeHabari

Serikali Yaanzisha Kitengo Cha Miliki Kutatua Migogoro Ya Ardhi

 Na Immaculate Makilika – MAELEZO Serikali imeendelea  kutambua maeneo yote yenye migogoro ya ardhi ili kuitatua kwa lengo la kuondoa ch...


 Na Immaculate Makilika – MAELEZO
Serikali imeendelea  kutambua maeneo yote yenye migogoro ya ardhi ili kuitatua kwa lengo la kuondoa changamoto hiyo kwa wananchi.

Akijibu swali jana Bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias Kwandikwa  alisema kuwa mgogoro wa ardhi kati ya Kambi ya Jeshi ya Itaka na  vijiji vya Itewe  na Sasenga vilivyopo jimbo la Mbozi, pamoja na mgogoro wa ardhi wa Kasulu imesababishwa na sababu mbalimbali  ikiwemo hali ya uzalendo iliyokuwa ikifanywa na jeshi hilo ya kuruhusu wananchi kufanya shughuli zao katika maeneo ya jeshi ambapo baadae wananchi wamehamia katika maeneo hayo.

“Nafahamu katika kambi ya Itaka kuna mgogoro wa ardhi na tayari Serikali  imetambua maeneo yote yenye migogoro ya  ardhi na tumejipanga kwa ajili ya kuitatua.  Tayari tumeanzisha kitengo maalumu cha Miliki ili kiweze kutatua maeneo yote yenye mgogoro ya ardhi nchini”, alisema Waziri Kwandikwa.

Aliongeza kuwa zoezi hilo litafanyika kwa kufuata utaratibu ili kuhakikisha kwamba haki inatendeka na wananchi wanapata  haki zao na jeshi linaendelea na shughuli zake kama kawaida.

Waziri Kwandika alisisitiza, “Zaidi ya asilimia 50 ya migogoro ya ardhi iliyopo kati ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali nchini na Jeshi la Kujenga Taifa imetatuliwa na maeneo mengi ambayo yalihitaji fidia wananchi wameshalipwa fedha zao, na hii inaonesha kuwa tunao mwendelezo mzuri wa kuendelea kulipa na hivyo tunatafuta fedha ili tuweze kulipa maeneo mengine yanayohitaji fidia”.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Serikali Yaanzisha Kitengo Cha Miliki Kutatua Migogoro Ya Ardhi
Serikali Yaanzisha Kitengo Cha Miliki Kutatua Migogoro Ya Ardhi
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiaYbeajhHCwwESGJCSrdByu3hCPIj105O4Zkj8mVHM3zBdvPJIk9j_KRcS0cYCBDMbVhZr-IqoV54d9qguEuoJwkT0A3DBySZFHUNhJH3eZei2YykpDSDPHujrNu8tWVScOkjx4v9gY9Iv/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiaYbeajhHCwwESGJCSrdByu3hCPIj105O4Zkj8mVHM3zBdvPJIk9j_KRcS0cYCBDMbVhZr-IqoV54d9qguEuoJwkT0A3DBySZFHUNhJH3eZei2YykpDSDPHujrNu8tWVScOkjx4v9gY9Iv/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/02/serikali-yaanzisha-kitengo-cha-miliki.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/02/serikali-yaanzisha-kitengo-cha-miliki.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy