Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa Simba ina wachezaji wazuri na wenye uzoefu wa kutosha kama wataamua kupambana wata...
Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa Simba ina wachezaji wazuri na wenye uzoefu wa kutosha kama wataamua kupambana watafika mbali kwenye mashindano ya Kimataifa (Caf Champions League)
Kaze amewapa nafasi Simba ya kufuzu robo fainali kama wachezaji wataamua kujituma na kupambana kwa ajili ya kutafuta matokeo kwenye mechi za makundi. Pia amewaomba mashabiki wa Simba na watanzania kwa ujumla kuisapoti Simba katika hatua hiyo.
“Moja ya faida kubwa ya timu kufika hatua za makundi , robo fainali , nusu fainali au fainali ni kutambulisha ubora wa ligi ya nchi husika.Hivyo tuwe sawa kuwaombea wenzetu hao kufanya vyema katika safari yao pia na wale wengine Namungo “
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS