FISTON Abdulazack, mshambuliaji mpya ndani ya kikosi cha Yanga amesema kuwa sababu kubwa ya kusaini mkataba ndani ya timu hiyo ni ukubwa ...
FISTON Abdulazack, mshambuliaji mpya ndani ya kikosi cha Yanga amesema kuwa sababu kubwa ya kusaini mkataba ndani ya timu hiyo ni ukubwa wa timu hiyo.
Fiston raia wa Burundi jana Januari 29 alitua Bomgo kumalizana na mabosi wake hao na amesaini dili la miezi sita.
Yeye ni mshambuliaji anaungana na kiungo mshambuliaji, Said Ntibanzokiza ambaye tayari ameshaanza kutumika ndani ya kikosi hicho.
Fiston amesema:"Nimesaini Yanga kwa kuwa ni timu kubwa na inajulikana nje na ndani ya nchi hivyo nami nimekuja pia kuungana na timu hii.
"Najua wengi wanapenda kuona nitafanya nini wasiwe na mashaka nitafanya vizuri na kila kitu kitakuwa sawa, ".
Yanga ipo nafasi ya kwanza chini ha Kocha Mkuu, Cedric Kaze ina pointi 44 baada ya kucheza mechi 18 ndani ya Ligi Kuu Bara.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS