Ghasia za kisiasa huko Sudan Kusini zapelekea watu kukosa makazi Watu wasiopungua 18 waliuwawa katika mgogoro wa silaha uliozuk...
Vifo hivyo vimewahusisha wafanyakazi wawili wa kundi la Madaktari wasio na mipaka-MSF waliopo Sudan Kusini ambao walishambuliwa katika nyumba zao, taasisi hiyo ilisema.
Timu zilifanya kazi usiku kucha kuwahudumia majeruhi 36 kwenye hospitali ya MSF mjini Malakar ilisema wagonjwa wasiopungua 25 walikuwa na majeraha ya risasi na wanane walihitajika kufanyiwa upasuaji. Maiti zaidi zinaendelea kuwasili hospitalini hapo.
Ghasia hizi awali ziliwalazimisha kiasi cha watu 600 wengi wanawake na watoto kukusanyika ndani ya hospitali.
Wengi wanakuja kutoka maeneo ambayo hayakupata msaada kwa miezi kadhaa wanawasili bila vifaa vyovyote.
COMMENTS