Coutinho akiifungia Liverpool bao la kusawazisha. Klabu ya Chelsea imekubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa vijogoo ...
Coutinho akiifungia Liverpool bao la kusawazisha.
Klabu ya Chelsea imekubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa vijogoo wa Anfield, klabu ya Liverpool, katika mechi ya EPL iliyopigwa kwenye dimba la Stanford Bridge, maarufu kama ‘darajani’.
Chelsea walipata bao la kuongoza dakika ya nne tu baada ya mchezo huo kuanza kupitia kwa Ramires na kabla ya kipenga cha half-time, Philippe Coutinho akaisawazishia bao Liverpool dakika ya 45.
Coutinho akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kufunga bao la pili.
Kipindi cha pili Chelsea walionekana kuelemewa katika mchezo huo kutoka na mashambulizi yaliyokuwa yakifanywa na Liverpool yaliyozaa bao la pili kutoka kwa Coutinho na baadaye Benteke akaihakikishia Liverpool pointi tatu kwa kutia kambani bao la tatu dakika ya 86.
Christian Benteke akiifungia Liverpool bao la tatu.
Baada ya kipigo hicho kibarua cha Kocha Jose Mourinho kinaripotiwa kuwamashakani kutokana na shinikizo kubwa analolipata kutoka kwa wamiliki na mashabiki wa klabu wanaotaka aachishwe kazi kutokana na muendelezo wa matokeo mabaya anayoyapata na kikosi chake.
COMMENTS