Mapacha ambao huwezi kubaini tofauti yao kwa haraka Lucy na Anna ni mapacha ambao wanatokea jimboni Perth nchini A...

Mapacha ambao huwezi kubaini tofauti yao kwa haraka
Lucy na Anna ni mapacha ambao wanatokea jimboni Perth nchini
Australia, mapacha hawa wamekuwa wakifanya vitu vinavyofanana kila
wakati.

Lucy na Anna wakiwa wanajiremba
Kutokana na mwonekano wao mtangazaji mmoja wa televisheni kutoka japani amesema hawa ndiyo mapacha wa kipekee duniani.

Je mdau wangu wewe unaweza kuwatofautisha warembo hawa
Warembo hawa wameonekana kujizorea umaarufu duniani kutokana na
kufanana kisura,kufanya kazi moja kwenye kituo cha kuwatunza watu wazee,
kutumia akaunti moja ya facebook, kutumia kitanda kimoja, kupokea
mshahara mmoja pia kuchangia mapenzi kwa mpenzi mmoja.

Mapacha hao wakionesha tabasamu lao
Hata hivyo kwasasa mapacha hao wamealikwa katika mashindano ya
kutafuta mapacha wanaofanana kila kitu nchini Japani na kuna uwezekano
mkubwa kwa mapacha hao kuibuka washindi.

Mapacha hao wakiwa na mpenzi wao ambaye ni fundi umeme
COMMENTS