Achinja mpwawe, auawa na kuchomwa moto
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi
HomeHabariKitaifa

Achinja mpwawe, auawa na kuchomwa moto

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, wakazi wa Mtaa za Nsalaga jijini hapa, jana asubuhi...

Ukawa wagawana Majimbo 211
JK aonya wahujumu wa Katiba mpya
Wamiliki wa mabasi wacharukia nauli

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, wakazi wa Mtaa za Nsalaga jijini hapa, jana asubuhi walishuhudia matukio ya mauaji ya watu wawili ndugu, moja likiwa ni mtu aliyemchinja na kumtenganisha kichwa na kiwiliwili mtoto wa dada yake, kabla naye kuuawa kwa kupigwa mawe na kisha mwili wake kuchomwa moto.

Yonah Mwamwele (38), ndiye aliyekuwa wa kwanza kumuua mtoto Johnson Mwamwele (5) mtoto wa dada yake kwa kutumia sululu.

Lakini ghafla, naye alijikuta akivamiwa na kundi la watu wenye hasira na kuanza kumshambulia kwa ngumi na silaha za jadi yakiwemo mawe hadi kumtoa uhai, na kisha kuuteketeza kwa moto mwili wake.

Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi aliyesema tukio la kwanza lilitokea jana saa 5:30 asubuhi katika eneo hilo la Nsalaga.

Msangi alisema kabla ya kumuua mpwa wake, Mwamwele alikuwa anamkimbiza mtoto huyo aliyekuja kubainika kuwa ni wa dada yake ambaye aliamua kukimbilia kwenye nyumba inayoendelea kujengwa iliyopo mtaani hapo, ambapo ndani yake walikuwepo mafundi wakiendelea na ujenzi.

“Mafundi walipomuona mtoto huyo akiingia na kufuatiwa na Mwamwele, walijaribu kumsihi ili amuache mtoto huyo, lakini aliwatishia sululu aliyokuwa ameishika mkononi ambapo mafundi hao waliogopa na kurudi nyuma ambapo alipata nafasi ya kuingia ndani,” alisema Msangi.

Kwa mujibu wa Msangi, mara baada ya kuingia ndani ya nyumba hiyo, Mwamwele alimfuata moja kwa moja mtoto huyo na kumpiga kwa sululu shingoni na kufanikiwa kutenganisha kichwa na kiwiliwili cha mtoto huyo aliyeaga dunia papo hapo.

Aliongeza mafundi baada ya kuona hali hiyo, walianza kupiga mayowe ya kuomba msaada, ambapo ghafla kundi kubwa la watu lilijitokeza na kuanza kumfukuza Mwamwele ambapo walifanikiwa kumkamata na kuanza kumpiga na baadaye waliamua kumchoma moto hadi kuteketea na polisi walipofika eneo la tukio walimkuta tayari ameaga dunia.

Kamanda Msangi alisema baada ya kukamilisha kufanya mauaji hayo ya Mwamwele, wananchi hao wenye hasira walirudi kwenye nyumba alimofia mtoto Johnson na kuanza kuipiga mawe huku wakivunja vioo vya nyumba hiyo kwa mawe, sababu kuwa ikielezwa wahusika walishindwa kutoa msaada kwa mtoto aliyeuawa.

Alisema upelelezi unaendelea ili kuweza kutambua kiini cha Mwamwele kuamua kumfukuza mtoto huyo wa dada yake na kisha kumuua kinyama kwa sululu.

Chanzo Habari Leo
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Achinja mpwawe, auawa na kuchomwa moto
Achinja mpwawe, auawa na kuchomwa moto
http://www.habarileo.co.tz/images/resized/images/kamanda-ahmed-msangi_300_172.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2015/03/achinja-mpwawe-auawa-na-kuchomwa-moto.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2015/03/achinja-mpwawe-auawa-na-kuchomwa-moto.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy