Yanga mambo yake safi
Mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima (kulia) akiwatoka mabeki wa timu ya BDF XI ya Botswana, Bonolo Phuduhudu na Master Masitara wakati wa mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana. Yanga ilishinda mabao 2-0. (Picha na Fadhili Akida).
HomeMichezoKitaifa

Yanga mambo yake safi

Mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima (kulia) akiwatoka mabeki wa timu ya BDF XI ya Botswana, Bonolo Phuduhudu na Master Masitara w...




YANGA jana ilianza vema michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuifunga BDF X1 ya Botswana mabao 2-0 katika mechi ya kwanza ya raundi ya awali ya michuano hiyo.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga ijiweke kwenye mazingira mazuri ya kusonga mbele katika mechi ya marudiano itakayofanyika baada ya wiki mbili mjini Gaborone, Botswana.

Mchezaji wa zamani wa Simba, Amis Tambwe ndiye aliyekuwa shujaa wa Yanga jana baada ya kuifungia mabao yote mawili.

Tambwe alifunga bao la kwanza katika dakika kwanza ya mchezo huo kwa kichwa baada ya kuruka juu na kuuwahi mpira wa kona katikati ya mabeki wa BDF.

Katika kipindi hicho cha kwanza, BDF walionekana kucheza kwa kujilinda zaidi hali iliyomaanisha kwamba walikusudia kupata sare. Tambwe aliipatia Yanga bao la pili katika dakika ya 56 akifunga tena kwa kichwa hatua tatu kutoka lango la BDF.

Alifunga bao hilo baada ya kuunganisha pasi safi ya Mrisho Ngassa aliyewachanganya mabeki wa BDF. Kwa ujumla Yanga ilianza mechi hiyo kwa kasi kiasi cha kuipoteza BDF XI katika dakika 20 za kwanza kabla haijakaa sawa na kujaribu kufanya mashambulizi.

Washambuliaji wa Yanga mara kadhaa walifika langoni mwa BDF lakini walikosa umakini na kujikuta wakipiga juu ama kupiga michomo dhaifu iliyodakwa na kipa wa wapinzani wao.

Katika dakika 20 za mwanzo BDF XI ilifanya shambulizi moja la nguvu wakati Master Mastara alipoingia eneo la hatari, lakini alipiga shuti lililopaa juu.

Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kushambulia kwa kasi, huku BDF XI wakionekana kupoteza muda zaidi kwa kuhitaji matokeo yabaki kama yalivyo na hapo ndipo Tambwe alipowapachika bao la pili.

Dakika ya 64, 65 na 67 lango la BDF XI lilikuwa katika hekaheka, lakini Nadir Haroub, Andrey Coutinho na Haruna Niyonzima kwa nyakati tofauti walishindwa kutumbukiza mpira wavuni.

Kikosi cha Yanga kilipangwa hivi: Ally Mustapha, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Nadir Haroub, Salum Telela, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe/Jerry Tegete, Mrisho Ngassa na Andrey Coutinho/Kpah Sherman.
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Yanga mambo yake safi
Yanga mambo yake safi
http://www.habarileo.co.tz/images/resized/images/bdf-yanga_300_170.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2015/02/yanga-mambo-yake-safi.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2015/02/yanga-mambo-yake-safi.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy