Mapema mwishoni mwa juma lililopita Bobbi Kristina ambaye ni mtoto wa marehemu mwanamuziki wa Marekani Whitney Houston alianguka baf...
Mapema mwishoni mwa juma lililopita Bobbi Kristina ambaye ni mtoto wa marehemu mwanamuziki wa Marekani Whitney Houston alianguka bafuni na kukimbizwa hospitali huku hali yake ikielezwa kuwa ni mbaya na kutakiwa kukaa chumba cha uangalizi maalumu.
Imeelezwa kuwa hadi sasa hali yake bado ni mbaya na madaktari wanaomuuguza katika hospitali ya Emory University wamepoteza matumaini na sasa wanaiachia familia yake hatma ya maisha yake.
Bobbi Kristina akiwa na baba yake Bobby Brown
Baba wa mtoto huyo Bobby Brown ana imani na kupona kwa mwanawe kwani katika familia yao kuliwahi kuwa na mgonjwa ambaye alikua na hali mbaya kwa muda wa siku nane lakini alipona.
COMMENTS