KOCHA, Louis van Gaal amefyumu kisa amefananishwa na David Moyes baada ya kikosi chake cha Manchester United kuchapwa na Southampton kwe...
Van Gaal aliiponda Southampton kwamba ilikwenda kwenye mechi hiyo iliyofanyika Old Trafford kwa dhamira tu ya kupata sare, lakini Dusan Tadic aliwafungia bao katika dakika ya 69 na kubadilisha kila kitu huku waandishi wakimtibua Mdachi huyo kwa kumfananisha na Moyes.
Kilichotokea ni kwamba Moyes alivunja rekodi nyingi sana alipokuwa kocha wa kikosi hicho huku ushindi huo wa juzi wa Southampton ukiwa wa kwanza kuupata Old Trafford baada ya miaka 27 kupita.
Van Gaal aliumizwa zaidi baada ya kuelezwa kwamba pointi alizovuna hadi sasa msimu huu hazina tofauti yoyote na ilivyokuwa kwa Moyes wakati ligi hiyo ilipofika hatua hii.
“Kwa hivyo mlikuwa mnasubiri tu ili mseme kwamba nina pointi sawa na ilivyokuwa kwa David Moyes,” alisema Van Gaal huku akionekana wazi kukasirishwa na kitendo hicho.
Van Gaal pia alitetea uamuzi wake wa kumwondoa kikosini straika Radamel Falcao katika mechi hiyo ya kipigo ambacho kimetibua rekodi yao ya kucheza mechi 10 bila ya kupoteza.
Falcao hakuwapo hata kwenye benchi na Mdachi huyo alimjumuisha kinda James Wilson kikosini kuliko supastaa huyo wa Colombia huku kipigo hicho cha bao 1-0 kikiifanya Man United kushuka hadi kwenye nafasi ya nne na Southampton ikipanda nafasi ya tatu.
COMMENTS