NYOTA wa zamani wa Manchester United, Cristiano Ronaldo anayekipiga Real Madrid amesema anataka kumalizia soka lake katika kikosi ...
NYOTA wa zamani wa Manchester United,
Cristiano Ronaldo anayekipiga Real Madrid amesema anataka kumalizia
soka lake katika kikosi kimoja nchini Brazil.
Mchezaji huyo amesema siku zote
amekuwa akitamani kucheza Brazil na hilo litatimia wakati utakapofika.
Katika siku za karibuni kumekuwa na tetesi kuwa Manchester United
inataka kumrudisha nyota huyo lakini mtazamo wa Ronaldo ni tofauti
kabisa.
Mchezaji huyo alinukuliwa akitamani kuvaa jezi ya klabu ya Corinthians au Flamengo kwa sababu ana marafiki wengi Brazil.
Wiki iliyopita Ronaldo, 29,
alipata tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia mbele ya wapinzani wake wa karibu
Lionel Messi na kipa Manuel Neuer. Karibu nyota huyo atagonga miaka 30
kwa hiyo anaanza kuangalia maisha ya mbele atakapoamua kumaliza soka.
COMMENTS