Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, akiwa nchini Bulgaria, Januari, Jan. 15, 2015. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani,...
Bwana Kerry alisema hayo wakati wa ziara yake ya nchini Bulgaria, ikiwa ni siku moja baada ya shirika la kutetea haki za binadamu Amnesty International, kutoa picha za setelaiti zikionyesha uharibifu mkubwa uliofanywa na wapiganaji wa Boko Haram katika miji miwili.
Bwana Kerry amesema Boko Haram ni moja ya vikundi vibaya na vya kigaidi duniani.
Kundi hilo la kigaidi, limekuwa likifanya mashambulizi mfululizo nchini Nigeria, na Cameroun, huku likisababisha raia kadhaa kuyakimbia makazi yao.
COMMENTS