NI siku nyingine tena tunakutana katika Live Chumba cha Habari cha Global Publishers, na leo tunaye staa wa michano ya Hip ...
NI
siku nyingine tena tunakutana katika Live Chumba cha Habari cha Global
Publishers, na leo tunaye staa wa michano ya Hip Hop kutoka Arusha, John
Simon ‘Joh Makini’ambaye alianza kufahamika kuanzia miaka ya 2004/2005
alipotoka na wimbo wake wa Hao, Hawapendi na Chochote, pia ni mmoja kati
ya wasanii wanaounda Kundi la Weusi na ni memba wa River Camp
Soldiers.
Joh Makini akilonga na Global TV Online.
Katika mahojiano aliyoyafanya na Global TV Online hivi karibuni ambayo yataruka hewani kesho Jumatano katika kipindi cha Mtu Kati kupitia tovuti ya www.globaltvtz.com”www.globaltvtz.com Joh alifunguka;
Mwandishi: Unauzungumziaje muziki wa Hip Hop kwa ujumla?
Joh Makini: Muziki wa Hip Hop kwa Tanzania ndiyo muziki anzilishi kabla ya miziki yote hii inayosikika watu walikuwa wanarap baadaye ndiyo ikaja R&B ambayo haikuwa na soko, Bongo Fleva ilikuja kutokea baadaye, nimekuwa nikishiriki kwenye matamasha mengi na nimegundua wasanii wa Hip Hop wakipanda kwenye jukwaa kunakuwa na hali tofauti yaani muamko mkubwa tofauti na wasanii wengine.
Mwandishi: Kundi lenu la Weusi mpo watano lakini mara nyingi stejini mmekuwa mkionekana watatu yaani wewe, Nick wa II na G Nako ni kwa nini?Joh Makini: Tuko memba watano, mmoja ni daktari anafanya kazi Kahama anaitwa Bonta. Suala la Bonta kutokuwepo kwenye steji na kukosekana kwenye baadhi ya nyimbo za Kundi la Weusi hakuna tofauti yeyote tuko vizuri tu, Lord Eyez alikuwa amesimamishwa na ndiyo maana hakuonekana kwenye steji kwa mwaka jana lakini kwenye matamasha mawili ya kufungia mwaka na Weusi alionekana.
Mhariri wa Gazeti la Risasi Jumamosi, Erick Evarist (kushoto) akipozi na Joh Makini |
.
Mwandishi: Unapata changamoto zipi kwa kufanya kazi na mdogo wako katika kundi moja?
Joh Makini: Kwenye undugu kuna wakati unakaa pembeni, kazi inachukua nafasi yake na kinachotuongoza ni Mwenyezi Mungu, Upendo na kuheshimiana, kizuri ni kwamba tulipokutana kila mtu alikuwa anajitegemea kwa maana kila mtu ana biashara zake na tukifanya kazi ya kampuni tunakutana kama Weusi Kampuni na tunafanya. Nasikia faraja sana kuzaliwa na ‘Genious’ na kufanya kazi na Nick wa II ni baraka kwangu.

Mwandishi: Nitajie wasanii watatu wa muziki wa Hip Hop ambao unawakubali sana hapa Bongo.
Joh Makini: Wapo wengi sana siwezi kuwataja na hata nje wapo wengi kama G2, Nas, 50 Cent,2 Pac, Notorious BIG na wengine kibao.
Mwandishi:
Unawasaidia vipi wasanii chipukizi hasa kutoka Arusha ambako ndiyo
chimbuko lenu na kuweza kujiunga na Kundi la Weusi?Joh Makini: Tunataka
wasanii na siyo kila rapa ana uwezo wa kuungana na Weusi, milango yetu
iko wazi siku zote na hata ukija pale River Camp wapo ambao bado tuko
kwenye levo ya kuwapa ushauri lakini siyo kusema tutamchukua mtu na
kumpeleka studio kwa sababu bado hajafikia ile levo ya michano ambayo
sisi tupo.
Martha Mboma (kulia), Omary Mdose (kushoto) wakipozi na Joh Makini. |
Mwandishi:
Unazungumziaje suala la wasanii kwenda kushuti video nje ya nchi? Mfano
wasanii wengi kukimbilia nchini Afrika Kusini.Joh Makini: Suala la
wasanii kwenda kufanya video nje ya nchi mimi nalisapoti kwa sababu siyo
kitu kibaya kwa kuwa muziki hauna mipaka kwa hiyo watu wanapokwenda
kufanya video Afrika Kusini au Nigeria wanafuata ubora na kikubwa
ambacho kinawatoa wasanii wa Afrika Mashariki na wengine kufanya video
kule ni wazi kwamba madairekta wa Afrika Kusini wana mawasiliano moja
kwa moja na Trace TV, MTV na Channel O ambao wamekuwa wanasimamia na
ndiyo maana inakuwa rahisi.
Mwandishi: Ni dairekta gani mbali na Nisher ambaye unamkubali na upo tayari kufanya naye kazi?
Joh Makini: Fundi Samweli ambaye nimefanya naye ngoma moja tu redioni lakini bado nipo kwenye mchakato wa kufanya naye ngoma nyingine nyingi.
Joh Makini: Fundi Samweli ambaye nimefanya naye ngoma moja tu redioni lakini bado nipo kwenye mchakato wa kufanya naye ngoma nyingine nyingi.
Kigogo wa Kitengo cha IT Global, Clarence Mulisa akipozi na Joh Makini. |
Mwandishi: Mafanikio yapi umeyapata kupitia muziki?
Joh Makin: Muziki unaendesha maisha yangu, kijana kama mimi kwa akili nilizonazo kama ningezitumia tofauti nafikiri ningekuwa paka road. Namshukuru Mungu kwa kipaji nilichonacho, muziki umenikutanisha na watu wengi na kunipa heshima japo kuna vitu vingi ambavyo bado naudai.

COMMENTS