Kocha wa Congo Claude le Roy Mambo yameanza kuiva na joto kupanda katika michuano ya kombe la mataifa ya Africa maarufu kama A...
Mambo
yameanza kuiva na joto kupanda katika michuano ya kombe la mataifa ya
Africa maarufu kama AFCON na kikubwa zaidi hivi sasa timu zote zinazo
tia maguu Equatorial Guinea zinapaswa kutafuta mahala pa kuweka ubavu
kwani kwa sasa pa kulala ni shiida .
Kocha wa timu kutoka Congo
Claude Le Roy ,anathibitisha kuwa kwa upande wake washiriki kutoka
nchini mwake wapatao 35 hawana vyumba vya kulala.
Kubwa zaidi
Claude anasema hoteli waliyofikia haina hadhi na viwango vya msafara
wake, na mbaya zaidi hoteli waliyofikia ina uhaba wa maji na nyaya za
umeme ziko wazi zenye kutishia usalama wa watu wake waliofurika kwenye
hotel hiyo na watano kati yao hawajui watalala wapi.
Sintofahamu
hii haiko kwa timu ya Congo tu bali hata kwa timu kutoka Burkina Faso
,kwani kocha wao Paul Put, jicho lake limefanikiwa kuona vifaa duni
vilivyoandaliwa kwa michuano hiyo, na kupendekeza kwamba ikiwa hali ni
hiyo kuna sababu gani kuharakisha michuano hiyo na badala yake
waahirishe mpaka mwezi June mwaka huu.
Equatorial Guinea yenyewe
inakuwa mwenyeji wa michuano ya kombe la mataifa ya Africa kwa taarifa
ya papo hapo baada ya Morocco kuvuliwa haki ya kuwa mwenyeji wa michuano
hiyo mwezi November.
Morocco ilisita kuwa mwenyeji wa michuano
hiyo kwa muda wa wiki tatu kwa hofu ya masuala ya kiafya kufuatia
mripuko wa gonjwa la kutisha lililokuwa likiitatiza dunia Ebola .
Mechi
ya ufunguzi wa michuano hiyo itakuwa kati ya Congo na Equatorial Guinea
siku ya Jumamosi na mchezo huo utapigwa katika mji wa Bata.
Akizungumza
na BBC kocha Le Roy amethibitisha kuwa hali imeanza kutishia Amani
kwani hakuna pa kulala na kuna ugumu wa kupata mahali pa malazi kwa
maofisa wake na hata wachezaji wanaotakiwa wapumzike zaidi pia hawana pa
kulala.
Umeme nao ni majanga,kila kitu kiko nje nyaya hazijavaa
nguo zake,nikataka kuosha mikono yangu,hakuna maji.baadhi ya maafisa
wangu nao walianza kuuzunguka mji wa Bata kuangalia kama watabahatisha
pa kulala popote pale lakini imekuwa ngumu mno .
Uwanja wa Estadio de Bata utakuwa mwenyeji wa nusu fainali za michuano ya mwaka 2012.
Le
Roy akazidi kusema kuwa pamoja na wakati mgumu unaowakabili wa kusaka
malazi mpaka sasa hawajasaidiwa chochote na shirikisho la soka barani
Afrika- CAF ,nay eye pamoja na maofisa wake walifika mjini humo siku
moja kabla wakijihami wasije kumbwa na matatizo lakini hali imekuwa
mbaya zaidi.
Haya niyaonayo niliyategemea,na sihitaji hoteli ya hadhi ya nyota tano,nnachotaka ni mahala safi pa kulala basi
Pamoja
na hayo yote Le Roy amewataka wachezaji wake kuhakikisha wanashinda
katika kundi lao na hivyo watapata hotel nzuri ya kulala wakati
walioshindwa watakapokuwa wakirejea makwao .
Lakini wachezaji wake tayari wameanza kukata tamaa na hasira juu kutokana na maandalizi duni waliyokutana nayo.
Michuano hii itaanza kupigwa rasmi Jumamosi na kufikia tamati tarehe 8 mwezi February.
COMMENTS