Wataalam Wa Ujenzi Wa Uchukuzi Wa Tanzania Na DRC Wapewa Mwezi Mmoja Kukamilisha Taratibu Za Mradi

Serikali za Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zimetoa mwezi mmoja kwa wataalam wa sekta za ujenzi na uchukuzi kukamilish...


Serikali za Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zimetoa mwezi mmoja kwa wataalam wa sekta za ujenzi na uchukuzi kukamilisha taratibu za kupata Mkandarasi wa ujenzi wa miundombinu ya reli na barabara ili kuanza kutekeleza miradi hiyo.

Akizungumza mjini Kalemie nchini DRC wakati wa kusaini makubaliano ya awali ya ujenzi huo Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Tanzania, Prof. Makame Mbarawa, amesema ni wakati muafaka wa nchi hizo kuunganishwa na miudombinu hiyo ili kuchochea uchumi na kurahisisha shughuli za Uchukuzi baina ya nchi hizo.

“Mkataba huu tuliosaini  ni mwanzo wa makubaliano ya nchi hizi katika hatua za awali za utekelezaji wa mradi huu, hivyo hatua inayofuata sasa ni wataalam kutengeneza hadidu za rejea kuelekea kumpata mkandarasi na kutangaza zabuni” amesisitiza Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amesema kwa muda mrefu nchi hizo zimekuwa zikizungumza nadharia ya kuboresha miundombinu kwa manufaa ya nchi hizo na kusema ni wakati muafaka sasa wa kuhakikisha mzigo wote unaotoka DRC unasafirishwa kwa wakati kupitia bandari ya Dar es Salaam.

Naye Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi kutoka DRC, Okende Senga, amesema maboresho ya miundombinu kwa pande zote yatachangia kwa kiasi kikubwa mzigo mkubwa kusafirishwa na hivyo kufanya nchi hizo kuboresha mahusiano ya kibiashara na kukuza uchumi wa nchi.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Ushoroba wa kati Central Corridor (CCTTFA), Florian Okanju, amesema kuwa zoezi la kukamilisha hadidu za rejea litakamilishwa kwa wakati kwani imekuwa ni ndoto ya Wakala huo kuona biashara inafanyika bila vikwazo hususani katika masuala ya miundombinu.

Mkataba huo uliosainiwa baina ya Tanzania na DRC unahusisha maboresho ya miundombinu ya reli na barabara yenye urefu wa kilomita takribani 1200 itakayotoka mjini Kalemie mpaka Lubumbashi, uboreshaji wa Bandari ya Kalemie na Momba pamoja na ujenzi wa Meli katika ziwa Tanganyika.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends

COMMENTS

BLOGGER
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,2861,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Wataalam Wa Ujenzi Wa Uchukuzi Wa Tanzania Na DRC Wapewa Mwezi Mmoja Kukamilisha Taratibu Za Mradi
Wataalam Wa Ujenzi Wa Uchukuzi Wa Tanzania Na DRC Wapewa Mwezi Mmoja Kukamilisha Taratibu Za Mradi
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhcKnDemiVaCpbYMf6gWdwtFLfRlH43g5Bvon1R67sT18CWr1LBGREippk5Wof2T765tnKyC9MUh0TKeZCvZmj0ZCbf14LhIuWeWUFkKS8XRCONOpW1IfeaBCBZwWZDhlmO_3Ra1ZrB5dOEhTsLelmvcVP_e0NS3MmSsVc9LxHJHO6-0uuaMBoUoI9_qA/s16000/1(3).jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhcKnDemiVaCpbYMf6gWdwtFLfRlH43g5Bvon1R67sT18CWr1LBGREippk5Wof2T765tnKyC9MUh0TKeZCvZmj0ZCbf14LhIuWeWUFkKS8XRCONOpW1IfeaBCBZwWZDhlmO_3Ra1ZrB5dOEhTsLelmvcVP_e0NS3MmSsVc9LxHJHO6-0uuaMBoUoI9_qA/s72-c/1(3).jpg
Antagon Blog
http://antagonf.blogspot.com/2022/07/wataalam-wa-ujenzi-wa-uchukuzi-wa.html
http://antagonf.blogspot.com/
http://antagonf.blogspot.com/
http://antagonf.blogspot.com/2022/07/wataalam-wa-ujenzi-wa-uchukuzi-wa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy