Veta Iringa yajivunia miaka 30 ya mafanikio
HomeHabariTop Stories

Veta Iringa yajivunia miaka 30 ya mafanikio

Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Mkoani Iringa kimeadhimisha miaka 30 ya VETA na miaka 50 ya ufundi stadi huku ikijivunia mu...

Bilioni 10 kutekeleza mradi wa umeme vitongoji 90 mkoani Njombe
Habari kubwa Magazetini Kenya leo October 2, 2024
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo October 2, 2024

Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Mkoani Iringa kimeadhimisha miaka 30 ya VETA na miaka 50 ya ufundi stadi huku ikijivunia muitikio wa wananchi kujiunga na mafunzo mbalimbali yanayotolewa na chuo hicho.

Maadhimisho hayo ya siku mbili yamehitimishwa katika Chuo cha elimu ya mafunzo ya ufundi stadi Mkoani Iringa ambapo pia yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama cha mapinduzi ambapo Mkuu wa Chuo hicho Pasiens Nyoni amewataka wananchi kupata mafunzo rasmi kupitia VETA ili wapate vyeti vitakavyowafanya kutambulika maeneo mbalimbali katika fani zao kulingana na ujuzi waliosomea.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa VETA kanda ya Nyanda za juu Kusini Suzan Magani ameeleza kuwa ndani ya miaka 30, VETA imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani kuna ongezeko kubwa la wanafunzi wanaojiunga na mafunzo ya ufundi stadi kutokana na kuongezeka kwa vyuo sita kwa kuwa hapo awali kulikuwa na vyuo viwili pekee (Iringa na Songea) hivyo kwa sasa kufanya kuwa na idadi ya vyuo nane kwenye Mikoa ya kanda ya nyanda za juu kusini.

Nao baadhi ya wanafunzi wanaopata mafunzo mbalimbali chuoni hapo wameeleza furaha yao kwa uwepo wa VETA kwani mafunzo wanayopata yatawasaidia kujiajiri na kuendesha maisha yao baada ya kuhitimu.

Maadhimisho ya VETA na ufundi stadi kitaifa yanatarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere kuanzia Tarehe 18 hadi 21 Mwezi Machi mwaka huu.

Hatahivyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa SACP Allan Bukumbi amewataka madereva wa vyombo vya moto Iringa kuwa na utaratibu wa kuendelea kupata mafunzo ya vyombo hivyo ili kuongeza umahiri wa fani hiyo kulingana na daraja la leseni husika ili kuendana na mabadiliko ya sheria za barabarani zinazojitokeza.

Katika hatua nyingine Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Salim Abri ambaye ameshiriki darasa la mafunzo ya udereva, ameweka wazi kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa sababu yanasaidia zaidi kwa madereva waliopata mafunzo miaka mingi iliyopita hivyo kusaidia kuendana na kasi ya ongezeko la watumiaji wa vyombo vya moto.

VETA Mkoa wa Iringa leo imehitimisha maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwake na miaka 50 ya ufundi stadi huku ikijivunia kuongezeka kwa wanafunzi pamoja na ongezeko la vyuo kwenye mikoa iliyopo nyanda za juu Kusini.

 

The post Veta Iringa yajivunia miaka 30 ya mafanikio first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/QfmIVsG
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Veta Iringa yajivunia miaka 30 ya mafanikio
Veta Iringa yajivunia miaka 30 ya mafanikio
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2025/03/IMG-20250301-WA0071-950x633.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2025/03/veta-iringa-yajivunia-miaka-30-ya.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2025/03/veta-iringa-yajivunia-miaka-30-ya.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy