Wafungwa kuanza kupewa ujuzi gerezani na vyeti vinavyotambuliwa na Veta: Bashungwa
HomeHabariTop Stories

Wafungwa kuanza kupewa ujuzi gerezani na vyeti vinavyotambuliwa na Veta: Bashungwa

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innnocent Bashungwa amelitaka Jeshi la Magereza kusimamia kikamilifu mpango wa kuwapa ujuzi na mafunzo ya ...

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innnocent Bashungwa amelitaka Jeshi la Magereza kusimamia kikamilifu mpango wa kuwapa ujuzi na mafunzo ya ufundi stadi Wafungwa wanapokuwa Gerezani na watakaohitimu mafunzo kutunukiwa vyeti vinavyotambuliwa na VETA wakati wanapomaliza vifungo vyao ili kuwajengea uwezo kujitegemea wanaporudi katika jamii.

Bashungwa ameeleza hayo tarehe 14 Februari 2025 wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Dodoma ambapo amebainisha kuwa Jeshi hilo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi (VETA) litaanza utekelezaji wa mpango wa kuwapa mafunzo Wafungwa wanapokuwa Gerezani.

Bashungwa ameeleza kuwa mpango huo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Jeshi la Magereza wa kuwapo ujuzi wa ufundi stadi Wafungwa wanapokuwa wanatumikia vifungo yao pamoja kurasimisha ujuzi wanakuwa nao na kuwapatia vyeti.

“Mheshimiwa Rais alitoa maelekezo kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, kuwapa ujuzi (ufundi stadi) kwa kuwaendeleza wanaoingia gerezani na ujuzi, lakini wale wanaoingia hawana ujuzi kabisa, kuangalia namna ya kuwapa ujuzi ili wanapotokaa waweze kujikimu kimaisha” ameeleza Bashungwa

Aidha, Bashungwa amemshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuliboresha Jeshi la Magereza kwa kulipatia vifaa na vitendea kazi ikiwa ni pamoja na Mabasi saba ya kusafirisha maabusu ambayo ameyazindua.

Bashungwa baada ya kuzindua Mabasi ya kusafirisha Maabusu, amemtaka Kamishna Jenerali wa Magereza CGP Jeremiah Katungu na Menejimenti kusimamia na kutunza mabasi saba aliyozidua ili yaweze kutoa huduma kama ilivyokusudiwa.

Kadhalika, Bashungwa ameeleza kuwa Jeshi la Magereza limekuwa mstari wa mbele kutumia nishati safi ambapo hadi sasa Magereza yote nchini yanatumia nishati safi na salama ya kupikia wakati wa kuandaa chakula cha Wafungwa.

Kwa upande wake, Kamishna Jenerali wa Magereza CGP Jeremiah Katungu ameishukuru Serikali kwa kuliwezesha Jeshi la Magereza kununua magari mapya ikiwa pamoja ya Mabasi ya kusafirisha maabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani ili kuwasaidia watuhumiwa kesi zao kusikilizwa na haki kutendeka kwa wakati.

The post Wafungwa kuanza kupewa ujuzi gerezani na vyeti vinavyotambuliwa na Veta: Bashungwa first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/EHMbOGx
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Wafungwa kuanza kupewa ujuzi gerezani na vyeti vinavyotambuliwa na Veta: Bashungwa
Wafungwa kuanza kupewa ujuzi gerezani na vyeti vinavyotambuliwa na Veta: Bashungwa
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250215-WA0015-950x634.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2025/02/wafungwa-kuanza-kupewa-ujuzi-gerezani.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2025/02/wafungwa-kuanza-kupewa-ujuzi-gerezani.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy