TANROADS isimamie miradi ya CSR ijengwe kwa viwango
HomeHabariTop Stories

TANROADS isimamie miradi ya CSR ijengwe kwa viwango

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ameuagiza Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kuwasimamia Wakandarasi wote wanaojenga ...

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ameuagiza Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kuwasimamia Wakandarasi wote wanaojenga na kukarabati miradi ya maendeleo kwa jamii (CSR) hapa nchini ili iweze kukamilika kwa ubora.

Mhandisi Kasekenya, ametoa agizo hilo Mkoani Kigoma leo tarehe 11 Januari, 2025 wakati akikagua miradi ya ujenzi inayoendelea kutekelezwa kwenye Sekta ya Elimu, Afya, Maji na Masoko kwa ushirikiano baina ya Halmashauri za Buhingwe, Manyovu, Kibondo na TANROADS.

Miradi hiyo inayotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa Shule ya Bweni Buhingwe, Kituo cha mabasi na uzio wa soko Manyovu, Ujenzi wa visima vya maji Buhingwe na Manyovu, Ukarabati wa Hospitali ya Kasulu pamoja na ujenzi wa Hospital Makere na Kibondo.

“Miradi hii inasimamiwa na TANROADS, kwa ushirikiano wa Benki ya Afrika ambayo ilitoa fedha ili kuhakikisha inajengwa kwa viwango vya hali ya juu na kwa wakati ili viweze kutoa huduma kwa wananchi”, amesisitiza Mhandisi kasekenya.

Amefafanua kuwa miradi ya CSR, ni miradi ambayo inajengwa kwa fedha za uwajibikaji wa kampuni kwa jamii kama vile ujenzi wa visima vya maji, shule, hospitali ambavyo vimetekelezwa kwenye Ujenzi wa barabara ambazo zinaendelea kujengwa Mkoani humo.

Kwa upande wake, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kigoma, Mhandisi Narcis Choma, ameahidi kuwa kupitia TANROADS na Wilaya za Buhingwe, Kibondo na Manyovu watashirikiana kuhakikisha Miradi hiyo yote ya CSR inakamilika kwa muda uliopangwa.

 

The post TANROADS isimamie miradi ya CSR ijengwe kwa viwango first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/e4CzHm2
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: TANROADS isimamie miradi ya CSR ijengwe kwa viwango
TANROADS isimamie miradi ya CSR ijengwe kwa viwango
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2025/01/IMG-20250117-WA0015-950x713.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2025/01/tanroads-isimamie-miradi-ya-csr-ijengwe.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2025/01/tanroads-isimamie-miradi-ya-csr-ijengwe.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy