Mchekeshaji Eliud atua na helkopta Arusha,Watanzania watakiwa kwenda hifadhini
HomeHabariTop Stories

Mchekeshaji Eliud atua na helkopta Arusha,Watanzania watakiwa kwenda hifadhini

TANAPA imezindua Kampeni ya Shangwe la Sikukuu na TANAPA Arusha lengo likiwa ni kuhamasisha watanzania na wasio watanzania kutembelea Hifadh...

TANAPA imezindua Kampeni ya Shangwe la Sikukuu na TANAPA Arusha lengo likiwa ni kuhamasisha watanzania na wasio watanzania kutembelea Hifadhi za Taifa kipindi hiki cha msimu wa sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya 2025.

Akizingumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Jully Bede Lyimo anayeshughulia Maendeleo ya Biashara TANAPA alisema, “TANAPA tuna hifadhi za Taifa 21 ambazo ni miongoni mwa Hifadhi Bora Afrika na Dunia kwa ujumla na zipo karibu kila mkoa wa Tanzania. Hivyo ushiriki wa watanzania kuzitembelea mbali na kufurahia uasili pia mtazitangaza.

Aidha, Kamishna Jully aliongeza kuwa fedha za viingilio wanazotoa watanzania hao huchangia katika kuongeza pato la Taifa ambalo huenda moja kwa kwenye ujenzi wa miundombinu ya barabara, Viwanja vya ndege , ujenzi wa Hospitali na mashule.

Kwa zaidi ya miongo sita tangu kuanzishwa kwake, TANAPA imeendesha kampeni nyingi lengo likiwa ni kuhamasisha watanzania kujiwekea utaratibu wa kutembelea vivutio vya utalii vinavyopatikana ndani ya hifadhi hizo.

Kwa mwaka huu kampeni hii ya Shangwe la Sikukuu na TANAPA inalenga kupita ofisi moja baada ya nyingine, mtaa kwa mtaa, mlango kwa mlango kuhakikisha watanzania wengi wanahamasika kutembelea Hifadhi za Taifa Tanzania.

Uzinduzi wa Kampeni hii umeanza kwa maandamano ya matembezi ya miguu yaliyochukua takribani masaa 3 kupita katika viunga mbalimbali vya jiji la Arusha na kuishia viwanja vya Gymkhana ikiwahusisha TANAPA, Chuo cha Utalii cha Taifa, wadau mbalimbali wa utalii, Mchekeshaji Eliud Samwel, Waandishi wa Habari na wananchi mbalimbali.

 

The post Mchekeshaji Eliud atua na helkopta Arusha,Watanzania watakiwa kwenda hifadhini first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/39FrM2C
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Mchekeshaji Eliud atua na helkopta Arusha,Watanzania watakiwa kwenda hifadhini
Mchekeshaji Eliud atua na helkopta Arusha,Watanzania watakiwa kwenda hifadhini
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/12/IMG-20241213-WA0071-950x634.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/12/mchekeshaji-eliud-atua-na-helkopta.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/12/mchekeshaji-eliud-atua-na-helkopta.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy