Wataalamu wa manunuzi wapewa maagizo,Rushwa yapigwa marufuku
HomeHabariTop Stories

Wataalamu wa manunuzi wapewa maagizo,Rushwa yapigwa marufuku

Katibu Tawala Mkoa wa Arusha (RAS), Musa Miseile amewataka wataalamu wa ununuzi hapa Nchini(PSPTB), kuwa wazalendo kwa kuzingatia maadili, w...

Katibu Tawala Mkoa wa Arusha (RAS), Musa Miseile amewataka wataalamu wa ununuzi hapa Nchini(PSPTB), kuwa wazalendo kwa kuzingatia maadili, weledi, kanuni na taratibu katika kutekeleza majukumu yao ya Ununuzi.

 

Missaile ameyasema hayo leo wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wataalamu wa manunuzi yanayoendelea mjini hapa.

 

Mafunzo hayo yameandaliwa na Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi (PSPTB)na kushirikisha wataalamu wa sekta hiyo toka halmashauri zote na sekretarieti ya mkoa wa Arusha.

 

Miseile amewataka kujiepusha na vitendo vya rushwa na kujikita zaidi katika kusimamia kikamilifu fedha zote za umma zinazotengwa kwa ajili ya miradi mbalimbali.

 

“hakikisheni mnajifunza kwa umakini mkubwa kuandaa na kutunza mikataba, na mzingatie yaleyote mnayofunzishwa hapa ili mkitoka muende mkayatekeleze kwa vitedo”alisisitiza katibu Tawala huyo wa Mkoa.

 

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi hapa nchini (PSPTB) Godfred Mbanyi alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wataalamu hao juu ya sheria mpya ya ununuzi na namna ya kusimamia mikataba.

 

Alisema kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo katika maeneo mengi hapa nchini ni wataalamu wa ununuzi kufanya kazi pasipo kusajiliwa na bodi hyo jambo ambalo ni kinyume cha sheria na kuwataka wale wote ambao hawajasajiliwa wajisajili mara moja.

 

“Natoa wito kuzingatia sheria kanuni na taratibu za manunuzi katika kutekeleza majukumu yenu, na nawataka wale wote ambao hawajasajiliwa na bodi kujisajili haraka iwezekanavyo kwani iko kwa mujibu wa sheria na anayefanya kazi bila kusajiliwa anavunja sheria za nchi”alisema Mbanyi

 

Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Catherine Mwamasage ambaye ni Mkuu wa kitengo cha manunuzi kutoka TANAPA, aliipongeza PSPTB kwa kuwapatia mafunzo hayo na kusema kuwa yatawasaidia kupata maarifa zaidi na wataenda kuyafanyia kazi kwa vitendo. 

The post Wataalamu wa manunuzi wapewa maagizo,Rushwa yapigwa marufuku first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/yXm4gBQ
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Wataalamu wa manunuzi wapewa maagizo,Rushwa yapigwa marufuku
Wataalamu wa manunuzi wapewa maagizo,Rushwa yapigwa marufuku
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/11/IMG-20241120-WA0009-950x534.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/11/wataalamu-wa-manunuzi-wapewa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/11/wataalamu-wa-manunuzi-wapewa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy